Katika jamii za Wasomali; ukeketaji unahusisha kuondoa clit na labia za ndani, kisha hushona mlango wa uke na kubakiza sehemu ndogo ya kukojolea. Unapoolewa, upande wa mume huja kuhakiki kama bado pamezibwa kisha huitwa kungwi kucha uwazi sehemu hiyo; kwa kawaida Bi Harusi hukaa ndani miezi 3 kabla ya kuingiliwa na mume wake hadi apone kidonda.
Huu sio utani; jamii hizi nimeishi nazo kwa zaidi ya miaka miwili na kwa wana ndoa kukutana kimwili ni pale wanapotaka kutengeneza mtoto vinginevyo hakuna mapenzi katika hilo.
Kuna koo fulani miongoni mwa wasomali wanaochukuliwa kama jamii za hali ya chini; hawa hawaruhusiwi kutahiri mabinti zao. Na wanaume wengi huitahidi miongoni mwa wake zake aoe mmojawapo kutaka koo hizi na huyu ndie atakuwa nusura yake katika ndoa. Bahati mbaya kutokana na hadhi yao ndogo katika jamii, huchukuliwa kama vijakazi ndani ya familia.