Halafu mimi huwa najiuliza sana! Hawa wasanii wanashindwa hat kutunga filamu kali juu ya ukeketaji (wakaiandaa hata kwa miaka miwili) wakatoa kitu cha ukweli na hata wakapata tuzo za kimataifa, wanakalia kuigiza mafilamu ya "I LOVE YOU" kila siku huku yakiwa na subtitles zenye broken English?
Hata wasanii wa nyimbo pia nao wamo kwenye kundi hilo hilo!
Kwa kufanya hivyo wangeweza kutoa ujumbe mzito kwa jamii mbalimbali na kujipatia pesa nyingi pia! Lkn wanakalia kutengeneza filamu 4 tofauti kwa mwaka, kila baada ya miezi mitatu filamu na kila filamu ina part 1 na 2 ambazo hizo part 1 na 2 huwezi kuzitofautisha!