ILO: Mishahara iongezwe mara kwa mara

ILO: Mishahara iongezwe mara kwa mara

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi(ILO) limesema janga la #COVID19 limeawaathiri sana waajiriwa wenye mishahara midogo.

Kuepuka athari zaidi ILO imeshauri mishahara kurekebishwa mara kwa mara. Na vilevile kupandisha kima cha chini cha mshahara ili uendane na hali ya uchumi.

Wamesema kwa miaka kumi iliyopita ni 70% ya nchi ambazo takwimu zao wanazo ambao wamepandisha mishahara. Wamesema watu milioni 266 wanalipwa chini ya kiwango cha chini cha mshahara.

Hivyo wameshauri Kiwango cha chini cha mshahara kuwekewa sera itakuza uzalishaji.

Kuongeza mishahara ni kitu kizuri sana lakini mishahara haiwezi kuongezwa kisiasa sababu ongezeko la mshahara sio la mwezi mmoja, hiyo ni budget endelevu, ukimuongeza mtu umeongeza hakuna kurudi kupunguza

Na pia hii nyongeza ya mshahara kwa watumishi haiishii tuu kumgharimu mwajiriri mshahara na pensheni.
Hapa muajiri anatakiwa kulipia other salary costs ambazo hazimhusu mtumishi bali zinamhusu muajiri pekee

Kwa afya ya makampuni, sekta mbalimbali na waajiriwa ni muhimu kufanya maamuzi sahihi kwa hili maana ukikosea hapa unaweza ishia kupunguza kazi watumishi au kufukuza kazi watumishi au kufunga office kabisa
 
Pesa ya kuongeza mishahara hakuna ila pesa ya kununua ndege 2 trillions.
Hiyo taarifa inaihusu na Tanzania? Maana huku mpango wetu ni kununua ndege tu

Wakuu kununua ndege ni one-time cost sio sawa na nyongeza ya mshahara. Inawezekana budget ya kununua ndege kwa mwaka ikawa 2trilions wakati ikifanyika salary icrement kila mwezi ikahitajika 2trillions ambayo ni sawa na 12trillions kwa hiyo nyongeza tuu.

Kila mtu anatamani nyongeza lakini isiwe kisiasa..... ifanyike tathmini, kama muajiri anaona ataweza kulipa bila longolongo aongoze

Vinginevyo tutaongezwa mishahara halafu tutarudi kuleee kwenye kukaa miezi2 bila mshahara kitu ambacho ni hatari zaidi

Tunajua serikali wanalifikiria hili na hata rais alishaahidi basi tuchape kazi, tuongeze uzalishaji, tulipe kodi ili hata maamuzi yanapokuja tuongezwe kiasi kikubwa zaidi
 
Kuongeza mishahara ni kitu kizuri sana lakini mishahara haiwezi kuongezwa kisiasa sababu ongezeko la mshahara sio la mwezi mmoja, hiyo ni budget endelevu, ukimuongeza mtu umeongeza hakuna kurudi kupunguza

Na pia hii nyongeza ya mshahara kwa watumishi haiishii tuu kumgharimu mwajiriri mshahara na pensheni.
Hapa muajiri anatakiwa kulipia other salary costs ambazo hazimhusu mtumishi bali zinamhusu muajiri pekee

Kwa afya ya makampuni, sekta mbalimbali na waajiriwa ni muhimu kufanya maamuzi sahihi kwa hili maana ukikosea hapa unaweza ishia kupunguza kazi watumishi au kufukuza kazi watumishi au kufunga office kabisa
Sisi nindona kantrii remember? Hatushindwi kuongeza mishahara hata kama ni bajeti endelevu
 
Huo ndiyo ukweli Mkuu.
Unajua tunazinguana nchi imeshika uelekeo wa kwenda shimoni bado tunawaaminisha wananchi kuwa tutazama kidogo then tutaibuka kumbe hizo nguvu za kuibuka hatuna na kama tunazo kwa nini tusizuie kuzama humo shimoni.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi(ILO) limesema janga la #COVID19 limeawaathiri sana waajiriwa wenye mishahara midogo.

Kuepuka athari zaidi ILO imeshauri mishahara kurekebishwa mara kwa mara. Na vilevile kupandisha kima cha chini cha mshahara ili uendane na hali ya uchumi.

Wamesema kwa miaka kumi iliyopita ni 70% ya nchi ambazo takwimu zao wanazo ambao wamepandisha mishahara. Wamesema watu milioni 266 wanalipwa chini ya kiwango cha chini cha mshahara.

Hivyo wameshauri Kiwango cha chini cha mshahara kuwekewa sera itakuza uzalishaji.

"MITANO TENA" ataongeza Tu tumpe MITANO TENA.
 
Back
Top Bottom