ILO: Mishahara iongezwe mara kwa mara

ILO: Mishahara iongezwe mara kwa mara

Unachosema ni kweli kabisa Mkuu na ndiyo sababu huyo anayejiita mwendawazimu na makamongo yake ndani ya maccm yanahaha hata kufanya forgery ili hao COVID19 wawe Wabunge wa viti maalum ili wawazuge UN kwamba kamati za Bunge husika zinaongozwa na Wabunge wa upinzani ili Nchi isikose trillions.

Kuna pesa kibao Nchi imepata miezi michache kabla ya uchaguzi na nyingine wamekopa wanaulizwa wamezifanyia nini wanang’aa macho. Kama ulivyosema Nchi inaelekea shimoni na bila Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi basi tutanasa huko shimoni kwa miaka mingi ijayo.

Unajua tunazinguana nchi imeshika uelekeo wa kwenda shimoni bado tunawaaminisha wananchi kuwa tutazama kidogo then tutaibuka kumbe hizo nguvu za kuibuka hatuna na kama tunazo kwa nini tusizuie kuzama humo shimoni.
 
Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi(ILO) limesema janga la #COVID19 limeawaathiri sana waajiriwa wenye mishahara midogo.

Kuepuka athari zaidi ILO imeshauri mishahara kurekebishwa mara kwa mara. Na vilevile kupandisha kima cha chini cha mshahara ili uendane na hali ya uchumi.

Wamesema kwa miaka kumi iliyopita ni 70% ya nchi ambazo takwimu zao wanazo ambao wamepandisha mishahara. Wamesema watu milioni 266 wanalipwa chini ya kiwango cha chini cha mshahara.

Hivyo wameshauri Kiwango cha chini cha mshahara kuwekewa sera itakuza uzalishaji.

Kumbe
 
Back
Top Bottom