I'm addicted to Social Media (Jamii Forums)

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Habari wana JF.Addiction kwa kiswahili imenitoka kidogo.

Ila nathubutu kusema nimeathiriwa na mitandao ya kijamii yaani hata mwaka hujapita toka nimeijua JF Ila sasa imeshaniathiri yaani muda wote natamani kufungua nyuzi,kusoma comments na kuandika chochote.

Yaani situlii kila muda niko JF .Zamani nilikuwa naipenda Instagram,Youtube na Facebook Ila sasa hivi kila mara niko Jamii Forums yaani hata nikiwa niko kazini naona efficiency ya kazi inapungua sasa kwasababu ya JF.

Nimekuwa interested na MMU forums kwasababu Ina utani mwingi na Ina wacheshi wengi.

Najuta kuijua Jamii Forums ni ngumu kuiacha ni kama unapovuta madawa ya kulevya ugumu uliopo kwenye kuacha matumizi ya madawa ni sawa na ugumu ulivyo katika kuiacha JF.

Ila nitoe kongole kwa mwanzilishi wa JF imenisaidia hasa mimi ambaye sio muongeaji sana in real life kupata sehemu ya kumaliza stress kusema nayojua lakini kujifunza mambo mengi ambayo wale wasioijua JF hawayajui..
 
Welcome to the world. Wewe NI Kati ya watanzania wachache Sana waliobahatika kulijua jukwaa hili. Ila pole coz Sasa jf kwa asilimia 60 imeanza kuwa utopolo, wapuuzi ni wengi kuliko great thinkers. By the way addiction kwa kiswahili ni uraibu au uteja.
 
Kwanini unasema wapuuzi ni wengi?
 
rafiki angu kazini alikua akinilazimisha mda mrefu kujiunga jf ila sikuwahi, jana ndo nimejiunga niseme ukweli hakuna mtandao bora kama huu maana una kila kitu hitajika katika ufaham wa mwanadam
 
rafiki angu kazini alikua akinilazimisha mda mrefu kujiunga jf ila sikuwahi, jana ndo nimejiunga niseme ukweli hakuna mtandao bora kama huu maana una kila kitu hitajika katika ufaham wa mwanadam
Duh!jana karibu bwana
 
Pole sana my friend, lakini ujue kwamba kila kizuri hakikosi kasoro JF ni sehemu salama kwa kujifunza vitu mbalimbali lakini ukija upande wa addiction kila mtu ni muhanga but kama umechukua uamuzi wa kuacha fanya mazoezi ya kujiwekea limit, na baadae una-acha moja kwa moja...kila la kheri mkuu
 
Waraibu tupo wengi mkuu japo 80% tunasomaga bila kuchangia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…