BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,869
- 13,137
Tukiwa tunaendelea kushuhudia maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliyotokana na mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd, ni vizuri wakati huu kujadili maswala yanayohusu ubaguzi wa rangi huku tukiwa tumejikita zaidi kwenye kujenga zaidi.
Kupitia nyimbo ya Hip Hop iitwayo I'm not Racist mchanaji (Joyner Lucas) amewasilisha ujumbe kwa kuvaa uhusika wa pande mbili kama Mzungu ambaye analaumu aina ya maisha wanayoishi watu weusi na pia kama mtu mweusi anayejikuta mhanga(victim) kutokana na mfumo wa nchi ambao umejaa upendeleo kwa wazungu.
Japo kwa ufupi tujaribu kutafakari yaliyomo kwenye wimbo huo.
1. Mzungu anadai kuwa mtu mweusi anamtukuza 2Pac kama mungu wakati mzungu anasoma vitabu na kuwafutilia watu kama Einstein na Steve Jobs.
2. Mzungu anadai kuwa mtu mweusi hana future yuko bize na muziki, pombe madawa ya kulevya.
3. Mtu mweusi analalamika kuwa historia ya utumwa pamoja na mfumo wa kiserikali vimemuathiri kwani akiomba nafasi za kazi hapati na ndo maana analazimika kuuza madawa ya kulevya ili kuweza kuishi.
4. Mtu mweusi anadai Wamarekani weupe hawakumpenda Barack Obama ndo maana wakamchagua Donald Trump ili waendeleze ubaguzi.
Mwisho wote wanaelewana na kuwa kitu kimoja(All lives matter).
Na ujumbe wa mwisho unatokea kuwa (Tulikuwa kitu kimoja mpaka pale pesa ilipotengeneza matabaka).