mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
"Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu" . Mithali 24:6
Kwa Mstari huu wa kwenye biblia acha nikupe kisa hiki kifupi na cha kipekee.
Twende kazi,
Mnamo tarehe 12 Februari 2008, wapo wanaume kadhaa walijipanga kwa siri kuzunguka jengo la apartmenti katika kitongoji kimoja cha kifahari huko Damascus.
Jioni ilipokaribia, waliona gari aina ya Mitsubishi Pajero la rangi ya silver likiwa limeegeshwa karibu na jengo hilo. Mwanaume mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi na mwenye ndevu zilizonyolewa vizuri alishuka kwenye gari hilo na kuingia ndani ya nyumba. Hakuwa ameandamana na walinzi wowote wale.
Maajenti waliokuwa wamejipanga barabarani waliinong’onezana kupitia vifaa vyao vidogo vya mawasiliano kwamba “yule mtu” alikuwa amewasili Damascus na alikuwa akielekea kwenye apartmenti hiyo. Walijua kwamba mwanaume huyo alikuwa anaenda kukutana na mpenzi wake wa siri, Nihad Haidar, mwanamke mmoja raia wa Syria aliyekuwa akimsubiri ndani ya apartmenti. Mwanaume huyo alikuwa amembebea zawadi kadhaa huyu Nihad mrembo, ambaye alikuwa ametimiza miaka thelathini wiki hiyo.
Wapenzi hao walikaa kwa saa kadhaa ndani ya apartmenti ya kifahari waliyopewa kutumia na Rami Makhlouf, mfanyabiashara tajiri na binamu wa rais wa Syria, Bashar al-Assad.
Dakika chache kabla ya saa nne usiku, mwanaume huyo aliyevaa nguo nyeusi aliondoka kwenye jengo hilo na kuingia kwenye Pajero ile ya rangi ya silver. Alikuwa anaelekea kwenye mkutano katika nyumba ya siri iliyokuwa eneo la Kafr Soussa, ambako alikutana na wajumbe kutoka Iran, Syria, na Palestina.☠️☠️☠️💀💀💀 💣 .......
Sasa Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Express la London, maajenti waliokuwa wakimfuatilia huyu bwana walikagua picha mpya ya mwanaume huyo kwenye simu zao za mkononi ili kuhakikisha kuwa hakungekuwa na kosa lolote la utambulisho. Waliendelea kuwasiliana muda wote na kutoa taarifa ya kila hatua ya “mlengwa” kwenye kituo cha operesheni cha Mossad.
Alipotoka kwenye jengo alikokuwa ametumia saa kadhaa akiwa na Nihad, maajenti walipata nafasi nzuri ya kulinganisha uso wake na picha zilizokuwa kwenye simu zao. Wakathibitisha utambulisho wake kwa wenzao waliokuwa Damascus pamoja na makao makuu huko Tel Aviv.
Kulikuwa na Hali ya wasiwasi mkubwa iliyotanda ndani ya Mossad. Wakuu wa idara mbalimbali walikusanyika katika ofisi ya waziri mkuu wa wakati huo Meir Dagan, ambako vifaa vyote muhimu vilikuwa vimeandaliwa kwa ajili ya kufuatilia operesheni hiyo moja kwa moja.
Mwanaume huyo aliwasha Pajero na kuondoka.
“Anaelekea huko,” mmoja wa maajenti alinong’ona tena kwenye kipaza sauti chake kidogo................
Mwanaume aliyekuwa ndani ya Pajero ya silver alikuwa Imad Mughniyeh, mtu aliyekuwa ameacha historia ndefu ya umwagaji damu kwa miaka mingi.
Tarehe 15 Novemba 2001, baada ya shambulio la Minara Pacha ya World Trade Center, Federal Bureau of Investigation (FBI) ilitoa bango kubwa lililokuwa na orodha ya magaidi wanaotafutwa zaidi duniani. Bango hilo lilikuwa na nembo za FBI, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, na Wizara ya Sheria ya Marekani. Orodha hiyo ilikuwa na majina ishirini na mawili pamoja na picha zao.
Jina la kwanza kwenye orodha hiyo lilikuwa la mtu aliyeonekana kuwa hatari kuliko wote. Dau ya dola milioni tano ilikuwa imetolewa kwa yeyote ambaye angewezesha kukamatwa kwake. Kabla ya mashambulizi ya Minara Pacha, alihesabiwa kuwa gaidi aliyesababisha vifo vya Wamarekani wengi zaidi kuliko gaidi mwingine yeyote aliyekuwa bado hai. Mtu huyo alikuwa Imad Mughniyeh. Faili lake la uhalifu lilikuwa zito sana. Na lilikuwa kama ifauatavyo yeye akiwa kama mastermind.
Aprili 18, 1983 — shambulio la bomu dhidi ya ubalozi wa Marekani huko Beirut, Lebanon: watu 63 waliuawa.
Oktoba 23, 1983 — bomu lililipuka katika makao makuu ya wanamaji wa Marekani huko Beirut: watu 241 waliuawa.
Oktoba 23, 1983, siku hiyo hiyo — bomu katika makao ya wanajeshi wa Ufaransa huko Beirut: watu 58 waliuawa.
Pia alihusishwa na kutekwa na kuuawa kwa afisa wa Central Intelligence Agency, William Buckley.
Pia Mashambulizi kadhaa dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Kuwait.
Utekaji wa ndege ya shirika la TWA pamoja na ndege mbili za shirika la ndege la Kuwait.
Mauaji ya Kanali William R. Higgins wa kikosi cha waangalizi wa Umoja wa Mataifa Kusini mwa Lebanon.
Mauaji ya wanajeshi ishirini wa Marekani nchini Saudi Arabia.
Orodha hiyo ilipofikishwa Israel, Mossad iliongeza taarifa zake kumhusu huyu imad:
Novemba 4, 1983 — bomu katika makao makuu ya jeshi la Israel huko Tyre, Lebanon: watu 60 waliuawa.
Machi 10, 1985 — shambulio dhidi ya msafara wa jeshi la Israel karibu na mpaka wa Israel na Lebanon: wanajeshi 8 waliuawa.
Machi 17, 1992 — bomu katika ubalozi wa Israel nchini Argentina: watu 29 waliuawa.
Julai 18, 1994 — bomu katika kituo cha jamii ya Wayahudi huko Buenos Aires: watu 86 waliuawa.
Pia alihusishwa na kutekwa na kuuawa kwa wanajeshi watatu wa Israel katika eneo la mpaka la Har Dov.
Kutekwa kwa mfanyabiashara wa Israel, Elhanan Tannenbaum.
Shambulio la bomu karibu na kibbutz ya Matzuba.
Na tukio lililoonekana kuwa kubwa zaidi: kutekwa na kuuawa kwa wanajeshi Ehud Goldwasser na Eldad Regev kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, jambo lililosababisha kuanza kwa Vita vya Pili vya Lebanon mwaka 2006.
Imad Mughniyeh, aliyekuwa akionekana kama gaidi mkuu nyuma ya matukio hayo yote, alikuwa kama mzimu. Alikuwa akisafiri mara kwa mara kati ya miji mbalimbali ya Mashariki ya Kati. Aliwakwepa wapiga picha na hakupenda kutoa mahojiano kwenye vyombo vya habari.
Mashirika ya kijasusi ya Magharibi yalijua mengi kuhusu shughuli zake, lakini yalijua mambo machache sana kuhusu sura yake halisi, tabia zake binafsi, na maficho aliyokuwa akiyatumia.
Walijua kwamba Imad Mughniyeh alizaliwa mwaka 1962 katika kijiji kimoja Kusini mwa Lebanon. Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zimekusanywa vipandevipande, wazazi wake walikuwa Washia wenye msimamo mkali wa kidini. Akiwa kijana mdogo, alihamia Beirut na kukulia katika mtaa maskini uliokuwa umejaa zaidi Wapalestina waliokuwa wafuasi wa Palestine Liberation Organization (PLO).
Aliacha shule ya sekondari na kujiunga na Fatah, tawi la kijeshi la PLO. Baadaye akawa mlinzi binafsi wa Abu Iyad, aliyekuwa naibu wa Yasser Arafat. Pia alijiunga na kikosi maalumu cha usalama cha Fatah kilichoitwa Force 17, ambacho kilianzishwa katikati ya miaka ya sabini na kuongozwa na Ali Hassan Salameh, maarufu kama “Red Prince(huyu salameh ndio aliyepanga mauaji ya waisraeli kwenye mashindano ya olimpiki huko ujerumani miaka ya 70 mwanzoni)
Lakini mwaka 1982, Israel ilianzisha vita vya Lebanon vilivyoitwa “Operation Peace for Galilee.” Jeshi la Israel lilivamia Lebanon na kuisambaratisha PLO. Wanachama waliobaki hai, wakiongozwa na Yasser Arafat, walipelekwa uhamishoni Tunisia.
Mughniyeh, hata hivyo, aliamua kubaki Lebanon na kujiunga na kundi la kwanza la waanzilishi wa Hezbollah.
Hezbollah, ambalo maana yake ni “Chama cha Mungu,” lilikuwa kundi la Kishia lililoanzishwa mwaka 1982 kama jibu la uvamizi wa Israel nchini Lebanon. Likiongozwa kiitikadi na Ruhollah Khomeini na kusaidiwa pamoja na kufundishwa na Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, Hezbollah lilikuja kuwa adui mkubwa wa Israel. Lengo lao kuu lilikuwa kuiondoa kabisa Israel kutoka Lebanon na hatimaye kuiangamiza.
Kuanzia siku za mwanzo kabisa za kuwepo kwake, Hezbollah ilijihusisha na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Israel. Na Mughniyeh alikuwa mtu aliyefaa kabisa kwa kundi hilo jipya kama mastermind.
Akiwa mtu aliyependa kufanya kazi gizani, alichagua kuendesha shughuli zake kwa siri na kuepuka kuonekana hadharani. Taarifa kuhusu yeye zilikuwa chache na mara nyingi zilipingana. Chanzo kimoja kilisema alikuwa mlinzi wa Muhammad Fadlallah, kiongozi wa kiroho wa Hezbollah, huku kingine kikidai kwamba alikuwa mkuu wa operesheni za kundi hilo na ndiye aliyepanga mashambulizi hatari zaidi yaliyosababisha mauaji makubwa.
Tofauti na aliyekuwa kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, Mughniyeh hakuonekana kwenye televisheni wala kutoa hotuba za chuki. Lakini ukweli usiopingika alikuwa hatari zaidi kuliko sheikh huyo aliyependa kuzungumza sana.
Kwa haraka alikua ni mmoja wa magaidi wenye uwezo mkubwa na waliokuwa wagumu zaidi kukamatwa duniani, sawa na Carlos the Jackal katika enzi zake, na kama mwenzake aliyemvutia sana, Osama bin Laden.
Mughniyeh alikuwa gaidi katili na mwenye mbinu za kipekee. Alijitokeza ghafla wakati alipopanga na kuongoza mauaji makubwa kadhaa nchini Lebanon mwishoni mwa Operesheni Peace for Galilee.
Alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja tu mnamo Oktoba 1983 alipowatuma washambuliaji wa kujitoa mhanga waliokuwa wanaendesha malori yaliyojaa mabomu kwenda kwenye makazi ya wanamaji wa Marekani na wanajeshi wa Ufaransa huko Beirut. Siku chache baadaye, alirudia mbinu hiyo dhidi ya makao makuu ya jeshi la Israel huko Tyre.
Akiwa na miaka ishirini na miwili, aliongoza kundi la magaidi kushambulia ubalozi wa Marekani uliokuwa na ulinzi mkali nchini Kuwait, na baadaye akateka ndege ya kwanza katika nchi hiyo.
Baada ya kila operesheni, alikuwa anatoweka kana kwamba ameyeyuka hewani.
Akiwa na miaka ishirini na mitatu, Mughniyeh aliteka ndege ya shirika la TWA iliyokuwa ikisafiri kutoka Athens kwenda Rome, na kumlazimisha rubani kutua katika uwanja wa ndege wa Beirut. Wakati wa utekaji huo, alimuua mwanamaji wa Marekani Robert Dean Stethem na kuutupa mwili wake nje kupitia mlango wa rubani.
Baada ya operesheni hiyo iliyodumu siku kumi na saba, Mughniyeh alifanikiwa kutoroka tena. Lakini safari hii aliacha kumbukumbu moja muhimu nyuma yake — alama zake za vidole ndani ya choo cha ndege.
Kiuhalisia hakuna kitu au jambo lilichojulikana kuhusu maisha binafsi ya Imad Mughniyeh, isipokuwa kwamba alikuwa amemuoa binamu yake, ambaye alimzalia mtoto wa kiume na wa kike.
Akiwa bado kijana sana, alitambua kwamba alikuwa akitafutwa na mashirika kadhaa ya kijasusi ya Magharibi, hivyo alijitahidi kuficha utambulisho wake. Alifanyiwa upasuaji mdogo wa kubadilisha sura nchini Libya, akaacha ndevu zikue, na akaepuka kuonekana hadharani.
Ni picha moja tu iliyothibitishwa ya Mughniyeh iliyowahi kufika mikononi mwa mashirika ya kijasusi ya Magharibi. Katika picha hiyo alikuwa mnene, mwenye ndevu, amevaa miwani na kofia yenye kivuli mbele.
Hata maelezo yake yalikuwa na makosa. Federal Bureau of Investigation (FBI) ilimwelezea kama: “Mzaliwa wa Lebanon, anayezungumza Kiarabu, mwenye nywele na ndevu za kahawia, urefu wa futi 5 na inchi 8 (sawa na sentimita 170), na uzito wa pauni 120 (karibu kilo 60).”
Ilikuwa vigumu kuamini jinsi mtu mwenye mwili mkubwa kama Mughniyeh angeweza kuonekana kana kwamba ana uzito wa kilo 60 tu. Maelezo hayo yalionyesha wazi jinsi alivyokuwa hodari katika kujificha na kuwapotosha maadui wake.
Baada ya mashambulizi yote, milipuko, na utekaji wa ndege alioufanya, alikuja kuwa shujaa anayeheshimiwa sana ndani ya Hezbollah. Alisifiwa kwa ujanja wake, ujasiri wake, na uwezo wake mkubwa wa kupanga operesheni, jambo lililofanya tawi la kijeshi la Hezbollah kuogopwa na mashirika ya kijasusi duniani.
Kadiri nguvu yake ilivyoongezeka, ndivyo alivyozidi kuwa TARGET 🎯 kubwa ya majaribio ya kuuawa na Israel pamoja na mataifa ya Magharibi.
Mughniyeh alitambua hilo, na akawa mtu mwenye hofu kubwa na mashaka ya kudumu. Aliishi maisha ya kukimbia kila wakati. Alimshuku kila mtu, hata watu wake wa karibu. Alibadilisha walinzi wake mara kwa mara, na kila usiku alikuwa analala sehemu tofauti.
Safari zake kati ya Beirut, Damascus, na Tehran zilifanyika kwa usiri mkubwa sana.
Kwa mujibu wa wasifu uliotayarishwa na Israel pamoja na mashirika mengine ya kijasusi, Mughniyeh alikuwa mtu aliyependa kujitenga, mwenye mvuto mkubwa wa ushawishi, mwenye kufanya maamuzi ya haraka bila kufikiri sana, na mwenye ujuzi mkubwa wa vifaa vya kisasa vya kielektroniki.
Alikuwa na uwezo wa ajabu wa kubadilisha utambulisho na mwonekano wake, jambo lililomsaidia kuwadanganya maadui wake mara kwa mara. Maajenti wa Israel walimpa jina la utani: “Gaidi mwenye maisha ya aina tisa.
Msako dhidi ya Mughniyeh uliendelea kwa miaka mingi.
Mwaka 1988, alikaribia kukamatwa na mamlaka za Ufaransa wakati ndege aliyokuwa akisafiria ilisimama Paris. Central Intelligence Agency (CIA) ilikuwa imewapa Wafaransa taarifa kuhusu Mughniyeh, ikiwemo picha yake na maelezo ya pasipoti bandia aliyokuwa akitumia.
Lakini Wafaransa waliogopa kwamba kukamatwa kwake kungeweza kusababisha kuuawa kwa mateka wa Kifaransa waliokuwa wanashikiliwa Lebanon wakati huo. Kwa hiyo wakaamua kupuuza uwepo wake na kumruhusu aondoke.
Mashirika ya Marekani yalijaribu pia kumkamata Ulaya mwaka 1986 na Saudi Arabia mwaka 1995, lakini kama kawaida yake, alitoweka bila kuacha alama.
Katika miaka hiyo, Imad Mughniyeh alikuwa akihusika kwa kiwango kikubwa katika kupanga na kutekeleza mashambulizi dhidi ya Waisraeli na Wayahudi nchini Argentina. Mwaka 1992, alipanga shambulio la bomu dhidi ya ubalozi wa Israel mjini Buenos Aires, kwa kutumia lori lililojazwa vilipuzi na kuendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga. Watu ishirini na tisa waliuawa. Baadhi ya viongozi wa Mossad waliona operesheni hiyo kama kisasi cha kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah, Sheikh Abbas al-Musawi, ambaye aliuawa katika shambulio la helikopta kusini mwa Lebanon.
Miaka miwili baadaye, shambulio jingine la bomu lilitikisa tena Buenos Aires, safari hii likilenga kituo cha jamii ya Kiyahudi, na kusababisha vifo vya watu themanini na sita. Kwa mara nyingine, baadhi ya wataalamu waliamini kuwa Hezbollah ilikuwa ikilipiza kisasi kwa kutekwa na Israel kwa mmoja wa viongozi wake nchini Lebanon, Mustafa Dirani.
Maafisa wa ujasusi kutoka Marekani na Israel waliokwenda Buenos Aires kuchunguza mashambulizi hayo mawili walihitimisha kuwa yalikuwa na uhusiano. Namna ya utekelezaji ilikuwa ileile: lori kujazwa vilipuzi na kuelekezwa kwenye target likiendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga. Mughniyeh alikuwa ametumia mbinu hiyo hiyo mjini Beirut na Tyre mwanzoni mwa shughuli zake.
Wachunguzi walibaini pia kuwa idara za siri za Iran pamoja na washirika wao wa ndani walihusika katika mashambulizi hayo.
Angalau moja ya malori yaliyotumika, lile lililoshambulia ubalozi, lilikuwa limeuzwa kwa magaidi hao na muuzaji wa magari wa Kishia kutoka Buenos Aires aitwaye Carlos Alberto Telleldín. Ushahidi ulielekeza waziwazi kwa Imad Mughniyeh.
Katika kipindi hicho, Mughniyeh alitumia muda mwingi nchini Iran. Baada ya kuuawa kwa Sheikh Abbas al-Musawi, aliogopa kuwa Israel ingejaribu kumuua pia. Akiwa mjini Tehran, aliunda kikosi maalum cha operesheni kilichojumuisha wapiganaji wa Hezbollah na maafisa wa ujasusi wa Iran. Washirika wake katika kuanzisha kikosi hicho walikuwa kamanda mkuu wa Islamic Revolutionary Guard Corps, Mohsen Rezaee, pamoja na waziri wa ujasusi Ali Fallahian. Inaonekana kikosi hicho hicho ndicho kilichotekeleza mashambulizi hayo mawili mabaya ya Buenos Aires.
Mashambulizi hayo yalikuwa na matokeo makubwa: Mughniyeh akawa mtu anayesakwa zaidi na Israel. Kwa matendo yake, alijihukumu mwenyewe kifo, ingawa ilichukua miaka mingi kabla hukumu hiyo kutekelezwa.
Mnamo Desemba 1994, Mughniyeh alionekana Beirut, na muda mfupi baadaye alinusurika jaribio la kumuua kwa kutumia gari lililotegwa bomu katika kitongoji cha kusini mwa mji huo. Polisi wa Lebanon walitoa taarifa haraka kwamba bomu lilikuwa limewekwa chini ya gari lililokuwa limeegeshwa karibu na msikiti ambako Sheikh Muhammad Fadlallah alikuwa akitoa hotuba yake. Mlipuko huo uliharibu duka la ndugu yake Imad, Fuad Mughniyeh, na mwili wake ulipatikana chini ya vifusi.
Lakini Imad mwenyewe, ambaye alitakiwa kuwepo hapo, alibadilisha uamuzi dakika za mwisho na akaamua kutokwenda, hivyo akaokoka tena. Bahati yake ilimwokoa kwa mara nyingine.
Wiki chache baada ya mlipuko huo, vyombo vya usalama vya Lebanon kwa kushirikiana na Hezbollah waliwakamata raia kadhaa waliotuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo kama washirika wa Mossad.
Mshukiwa mkuu alikuwa mtu aitwaye Ahmed Halek. Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya polisi, “Halek na mke wake waliegesha gari lao karibu na duka la Fuad Mughniyeh. Halek aliingia dukani kuhakikisha kuwa Fuad alikuwepo, akamsalimia kwa kupeana mkono, kisha akarudi garini na kuwasha bomu.”
Gazeti la Lebanon la AS-SAFIR, likinukuu vyanzo vya kuaminika, lilisema kuwa Halek alikuwa ameshiriki mkutano na afisa mwandamizi wa Mossad huko Cyprus. Afisa huyo wa Mossad alimfundisha jinsi ya kutumia bomu hilo na akamlipa takriban dola 100,000. Baadaye Halek alikuja kuuawa na haikujulikana ni kwa hukumu ya kunyongwa au kupigwa risasi. Anyway....
Safari hii Imad Mughniyeh alinusurika tena, lakini maagent wa Mossad hawakukata tamaa. Walikusanya kwa makini kila taarifa ndogo waliyoipata kumhusu, wakaunganisha ripoti kutoka idara mbalimbali za ujasusi za kigeni, na kujifunza mbinu binafsi za Mughniyeh.
Mwaka 2002, Mossad ilipokea taarifa nyingine kuhusu Mughniyeh, ikimhusisha na usafirishaji wa tani hamsini za silaha kwa magaidi wa hamas wa Kipalestina. Lakini baadaye akapotea tena. Kulikuwa na uvumi kwamba alikuwa amekuwa kamanda mkuu wa Hezbollah na huenda ndiye angechukua nafasi ya Sheikh Hassan Nasrallah siku zijazo.
Uhusiano wake mkubwa ulikuwa na idara ya ujasusi ya Iran, na ilisemekana kuwa alikuwa akifanya kazi kwa karibu na Brigedi za Quds Force, ambazo zilikuwa na jukumu la kushirikiana na jamii za Washia duniani pamoja na mashirika ya kigaidi yanayoungwa mkono na Iran.
Cheo chake cha juu kilimlazimu kuongeza ulinzi wake binafsi. Kulikuwa na uvumi wa mara kwa mara kwamba alikuwa amebadilisha tena sura yake, huenda kupitia upasuaji mwingine wa plastiki. Kwa mujibu wa vyanzo vya Ulaya, mwishoni mwa vita ya Lebanon 2006 , Mossad iliwaajiri Wapalestina kadhaa waliokuwa wanaishi Lebanon na waliokuwa wanaipinga sana Hezbollah.
Mmoja wao alikuwa na binamu katika kijiji alichotoka Mughniyeh. Mwanamke huyo alimwambia wakala mpya wa Mossad kwamba Mughniyeh alikuwa amesafiri kwenda Ulaya na kurudi Lebanon akiwa na uso tofauti kabisa. Hivyo Mossad ikapata changamoto mpya — kufanya upelelezi katika kliniki za upasuaji wa plastiki kote Ulaya.
Mafanikio yasiyotarajiwa yalitokea mjini Berlin. Kwa mujibu wa mwandishi wa Uingereza Gordon Thomas, agent wa Mossad mjini Berlin aliyeitwa Reuven alikutana na mtoa taarifa wa Kijerumani . Mtoa taarifa huyo(informer) alisema kuwa Imad Mughniyeh alikuwa amefanyiwa upasuaji kadhaa wa plastiki uliobadilisha kabisa sura yake.
Matibabu hayo yalifanyika katika kliniki ambayo zamani ilikuwa ikimilikiwa na STASI, idara ya siri ya kijasusi yaUjerumani Mashariki wakati huo. Stasi ilikuwa ikitumia kliniki hiyo kubadilisha nyuso za mawakala na magaidi waliotumwa kufanya operesheni za siri katika nchi za Magharibi.
Baada ya mazungumzo magumu, Reuven alikubali kumlipa mshirika huyo wa Kijerumani fedha nyingi, na akapokea faili lenye picha 34 mpya za Mughniyeh.
Uchambuzi wa picha hizo uliofanywa na wataalamu wa Meir Dagan ulionyesha kuwa Mughniyeh alikuwa amefanyiwa upasuaji wa taya: sehemu za taya yake ya chini zilikuwa zimekatwa na kupandikizwa upya kwa namna iliyofanya kidevu chake kuwa chembamba zaidi, hali iliyomfanya aonekane mwembamba na aliyedhoofika........
Inaendelea.......📌📌📌📌📌📌
eli -DEFIANT- cohen
MENEMENE TEKERI NA PERESI