Hujawahi hudhuria msiba WA mwenye Imani tofauti na yako?View attachment 3316806
Imam Mkuu wa Al-Azhar, Ahmed El-Tayeb, ambaye pia aliwahi kuwa Mufti Mkuu wa Misri, ni msomi mashuhuri wa dini ya Kiislamu, mwenye elimu, ujuzi, na uelewa mkubwa wa masuala ya dini na dunia kwa ujumla. Ni rafiki wa karibu wa Papa Francis, na amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kukuza maelewano kati ya Waislamu na Wakristo duniani. Katika ishara ya heshima kubwa kwa uhusiano wao wa kipekee, Ahmed El-Tayeb atahudhuria mazishi ya Papa Francis.
Uhusiano kati ya Al-Azhar University — taasisi ya Kiislamu ya elimu ya juu yenye makao yake mjini Cairo, Misri — na Roma kupitia Vatican, umeimarika kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha Papa Francis na Imam Ahmed El-Tayeb. Al-Azhar, ikijulikana kama mojawapo ya vituo vya kale zaidi vya elimu ya Kiislamu duniani, imekuwa mshirika muhimu wa Vatican katika kujenga majadiliano ya kidini (interfaith dialogue).
Katika miaka ya nyuma, kulikuwa na nyakati za mvutano kati ya Al-Azhar na Vatican, hasa baada ya matamshi yaliyohusiana na Uislamu kutolewa na Papa Benedict XVI mwaka 2006. Hali hiyo ilipelekea kusitishwa kwa muda majadiliano rasmi kati ya pande hizo mbili. Hata hivyo, mambo yalibadilika Papa Francis alipoingia madarakani mwaka 2013, akisisitiza juhudi mpya za kujenga madaraja ya maelewano.
Kwa kuonesha matunda ya juhudi hizo, mnamo Februari 2019, Papa Francis na Imam Ahmed El-Tayeb walikutana huko Abu Dhabi, na pamoja walitia saini hati muhimu sana ijulikanayo kama:
- "Document on Human Fraternity for World Peace and Living Together" (Hati ya Undugu wa Kibinadamu kwa ajili ya Amani ya Dunia na Kuishi Pamoja).
Hati hii ilihimiza:
- Amani kati ya mataifa na dini.
- Kuheshimu haki za binadamu.
- Kukemea vikali vitendo vya vurugu, ugaidi na ubaguzi wa aina yoyote.
Kwa msingi huo, Al-Azhar na Vatican walikubaliana pia kuanzisha:
- Kamati ya Kimataifa ya Undugu wa Kibinadamu ili kuendeleza malengo ya hati hiyo.
- Miradi ya elimu na mafunzo yanayohimiza kuheshimu tofauti na kuishi kwa maelewano.
Zaidi ya hapo, uhusiano wa karibu kati ya Ahmed El-Tayeb na Papa Francis umeendelea kuonekana kupitia:
- Mikutano mbalimbali ya kidini na kimataifa.
- Ushirikiano wa kielimu kati ya Al-Azhar na taasisi za Katoliki.
- Miradi ya pamoja ya kukuza maadili ya amani, haki za kijamii, na heshima kwa kila mtu.
Kwa hivyo, ushiriki wa Imam Mkuu Ahmed El-Tayeb katika mazishi ya Papa Francis si tukio la kawaida tu la kidiplomasia, bali ni alama kubwa ya undugu wa kidini na uhusiano wa kihistoria uliokomaa kati ya Al-Azhar na Kanisa Katoliki la Roma.
Story za abunuasi tu hizi na biblia ipo wazi na inasema giza na nuru kamwe havikai pamoja na amuaminiae mungu imempasa kunia amini na mimi (yesu) na mstari mwingine unasema wa mwabuduo mungu imewapasa kumwabudu kwenye roho na kweli na binadamu wanao mwabudu mungu wa kweli ni wale wanao abudu katika kanisa linalo fundisha injili ya kweli ya kristo yesu na sio vinginevyo au mahali pengineHakuna uadui kati ya uislam na ukristo. Ni baadhi tu ya mashetani wamejiingiza humo kwenye dini na kuzifanya dini kuwa viwanda vya kuzalisha mashetani.
Mungu ni upendo. Sasa unasikia jitu linamwua mwenzake huku likimtaja Mungu? Jitu linaenda kushambulia watu wa dini nyingine na kuwaua, halafu linasema eti linatimiza maagizo ya Mungu.
Yesu Kristo alisema kuwa amri kuu ni UPENDO.
Ukisikia kiongozi wa dini yoyote ile, anahubiri upendo na haki, usiitizame dini yake, ujue kuwa huyo ni mjumbe wa Mungu wa kweli.
Kuna mwombaji mmoja, mtumishi wa Mungu, anayejitahidi sana kuomba, yeye ni mlokole wa makanisa haya ya kiroho. Akasema kuwa, sijui nitawaambiaje wenzangu hadi wanielewe. Akasema, ' mimi siku zote nilikuwa napinga mambo ya kuwaombea wafu, na niliamini kabisa hakuna muislam anayemwabudu Mungu wa kweli. Lakini siku moja nikiwa nafanya maombi yangu ya kawaida, nilisikia sauti ikiniambia, hakuna sala yenye nguvu kwa marehemu kama sadaka ya misa inayotolewa na Kanisa Katoliki; halafu nikaambiwa, misikiti mingi inaendesha ibada za ibilisi, lakini kuna msikiti mmoja, msikiti wa ...... (nimesahau jina), unafanya ibada kamili ya Mungu wa kweli. Kuna baadhi pia ya makanisa, yanafanya ibada za ibilisi". Akasema kuwa toka siku hiyo analiheshimu sana Kanisa Katoliki, na wala hawezi kuwaona waislam kama alivyokuwa akiwaona hapo mwanzo.
Kwani unafikiri huyo imam hamuoni papa kafiri!?.. palikua na makafiri wengi tu chini ya mtume,akiwalinda kama mkuu wa dolaSasa utamkuta mfia dini kavaa kobazi yupo Nangurukuru hukoo anaita wenzie makafiri
Injili ya yesu iko wapi?..tunaona injili za akina mathayo, Marko etcStory za abunuasi tu hizi na biblia ipo wazi na inasema giza na nuru kamwe havikai pamoja na amuaminiae mungu imempasa kunia amini na mimi (yesu) na mstari mwingine unasema wa mwabuduo mungu imewapasa kumwabudu kwenye roho na kweli na binadamu wanao mwabudu mungu wa kweli ni wale wanao abudu katika kanisa linalo fundisha injili ya kweli ya kristo yesu na sio vinginevyo au mahali pengine
hilo la kafiri haliwezi kufutika mileleSasa utamkuta mfia dini kavaa kobazi yupo Nangurukuru hukoo anaita wenzie makafiri
Acha ufala dogo, kuzikana ni sehemu ya ibada, hata kiongozi wetu Mtume wetu alikuwa anaacha majukumu yake pale anapoona.watu wanaenda kuzika, naye anajiunga nao kwenda mazikoni.Sasa utamkuta mfia dini kavaa kobazi yupo Nangurukuru hukoo anaita wenzie makafiri
Ukijibiwa nistue.Injili ya yesu iko wapi?..tunaona injili za akina mathayo, Marko etc
Ila hata mtume Muhammad (SAW) mpaka anakufa alikuwa kafiri.Kwani unafikiri huyo imam hamuoni papa kafiri!?.. palikua na makafiri wengi tu chini ya mtume,akiwalinda kama mkuu wa dola
Injili mnayoiamini nyie ni hipi, na iko wapi?Injili ya yesu iko wapi?..tunaona injili za akina mathayo, Marko etc
Shida yenu, dini yenu mnaiendesha kwa akili zenuSasa utamkuta mfia dini kavaa kobazi yupo Nangurukuru hukoo anaita wenzie makafiri
Sisi mafundisho yetu tunayatoa kwa Mtume.Sasa utamkuta mfia dini kavaa kobazi yupo Nangurukuru hukoo anaita wenzie makafiri