Imani inayoongozwa na mapenzi au chuki hupofusha

Imani inayoongozwa na mapenzi au chuki hupofusha

Achanakia

Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
70
Reaction score
81
Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu imani yao kwa viongozi wetu wa nchi inatawaliwa zaidi na mapenzi yao au chuki yao kuliko uhalisia.

Mtu akishampenda kiongozi fulani kwasababu zake binafsi, basi kiongozi huyo hata akiwa anaboronga katika utendaji wake wa kazi, yeye ataona yuko sawa, hata akiwa anadanganya juu ya jambo fulani yeye ataona yuko sahihi kwa vile tu anampenda.

Kadhalika, akiwa na chuki juu ya kiongozi fulani badi hata kama huyo kiongozi atafanya vizuri yeye ataona huyo kiongozi hafai na anachokifanya ni upuuzi tu, kiongozi huyo akiongea jambo hata kama ni jambo la manufaa kiasi gani yeye ataona ni upuuzi na ni uongo.

Hapa nitatoa mfano moja uliodhahiri kuhusiana na rais wetu wa sasa Mama Samia na mtangulizi wake Hayati Magufuli kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo.

Wapenzi wa Magufuli wanamuona mama kama ni msaliti kuruhusu huo mradi kuendelea ili hali Magufuli alisema ni kichaa tu anayeweza kuukubali mradi huo kutokana na masharti yake. Hapa utaona kabisa wanaamini kabisa alichokisema Magufuli ulikuwa ni ukweli mtupu, lakini zaidi wakiongozwa na mapenzi yao kwa Magufuli, maana hawataki kabisa kujishughulisha kutaka kuuona huo mkataba ili wajiridhishe kama hayo alitoyasema Magufuli yana ukweli kiasi gani. (Ukiwauliza wanakupa jibu la jumla tu kuwa Magu alikuwa ni mzalendo namba moja kwa nchi yake)

Kwao chochote anachokifanya mama Samia wanaona kama ni usaliti na wanaenda mbali kwakusema mama hafanyi mambo kwa utashi wake, anaendeshwa na rais mstaafu JK. Hiyo yote ni chuki.

Upande mwingine wasiompenda Magufuli wanaona kila alichokuwa anakifanya kilikuwa cha hovyo na zaidi alikuwa ni mtu muongo sana.

Hivyo hata hayo masharti ya mradi kama alivyosema wanaona huo ulikuwa ni uongo wake tu kutaka kuhalalisha hoja yake ya kusitisha mradi. Wanasema yeye alikuwa na tabia ya kuponda miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake akisema ni miradi ya hovyo haina maslahi kwa taifa, lakini wakati huo hakuwa tayari kuonyesha mikataba ya miradi aliyoianzisha yeye ili watu wajue masharti yake yakoje. Na mara nyingi miradi yake haikushirikisha bunge na haikufuata utaratibu wa tenda za manunuzi.

Je, kwa mitazamo ya haya makundi tunatokaje? Nini kifanyike ili kujenga imani ya kweli isiyoongozwa na mapenzi binafsi kwa viongozi?

Je, iko haja sasa ya kubadili sheria zetu ili hiyo mikataba isiendelee kuwa siri?
 
Huwezi kubadili hiyo ndio tafsiri ya siasa hapa kwetu ila kuhusu Mama samia sio kwamba wanampenda bali ni kama wanamshabikia kwa sababu ya kuwaudhi wapenz wa Magufuli.

Muhimu nachokushauri ni kwamba usiwachukulie serious kwa sababu hata wao hawako serious wanachofanya ni kama sehemu ya kujiburudisha tu.
 
Upande mwingine wasiompenda Magufuli wanaona kila alichokuwa anakifanya kilikuwa cha hovyo na zaidi alikuwa ni mtu muongo sana.
Hujakosea. Magufuli alikuwa muongo, mzandiki na mfitini.

Mifano:
- Alisema tunajenga miradi ya kimkakati kwa fedha zetu za ndani. Ni kweli tunatumia fedha za ndani?

- Alisema ndege tulizonunua zimeanza kuleta faida. Na akafanya na bongo movie ya kukabidhiwa gawio. Ni kweli zinaleta faida?
 
Back
Top Bottom