Imani Kajula aomba kuachia ngazi ya Mtendaji Mkuu (CEO) Simba. Je, ni dalili ya kurejea kwa Barbara Gonzalez?

Robidinyo

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
4,043
Reaction score
8,686
TAARIFA KWA UMMA

Imani Kajula aomba kuondoka klabuni hapo
20240715_171928.jpg

Klabu ya Simba inapenda kuujulisha umma kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imeridhia maombi ya Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula kuomba kuondoka ifikapo mwisho mwa mwezi Agosti 2024 mkataba wake utakapoisha.

Kufuatia maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba inafanya jitihada za kupata Afisa Mtendaji Mkuu mpya. Umma utapewa taarifa zoezi hili litakapokamilika.

Pamoja na uamuzi huu, Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula anaendelea na majukumu yake ya kiutendaji kikamilifu hadi tarehe 31 Agosti 2024.

Imetolewa na:
Idara ya Habari na mawasiliano, Klabu ya Simba.
15 Julai, 2024

Pia soma:
 
1721056819138.png

Bodi ya Wakurugenzi Simba SC imekubali maombi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wao Imani Kajula ya kuachia ngazi ndani ya Simba SC kuanzia Agosti 31- 2024 huku klabu hiyo ikianza mchakato wa kutafuta Mtendaji Mkuu ndani ya wababe hao wa Msimbazi.

Kajula aliingia Simba mnamo Januari 2023 na kusaini kandarasi ya miezi 6 uliokuwa na kipengele cha kuongeza muda huku alirithi mikoba ya Barbara Gonzalez aliyeondoka ndani ya Simba SC kipindi hicho.

Kajula anaondoka ndani ya Simba SC akishinda kombe la Muungano 2024 pamoja na Ngao ya Jamii msimu 2023-24,kufika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika 2023-24 pamoja na kuanzisha mifumo bora ya Wanachama kama Simba Executive Network kwa ajili ya kuiongezea mapato ndani ya klabu hiyo.
 
Nadhani Barbra anarudi nae ni my wetu yanga tunampenda mno Kuna Raha kupiga team ya CEO mrembo
 
Dada Barbara Gonzalez ameshamaliza likizo yake ya uzazi sasa hv anarudi mjengoni...utopwenga kazi mnayo
 
Bodi ya Wakurugenzi Simba SC imekubali maombi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wao Imani Kajula ya kuachia ngazi ndani ya Simba SC kuanzia Agosti 31- 2024 huku klabu hiyo ikianza mchakato wa kutafuta Mtendaji Mkuu ndani ya wababe hao wa Msimbazi.

Kajula aliingia Simba mnamo Januari 2023 na kusaini kandarasi ya miezi 6 uliokuwa na kipengele cha kuongeza muda huku alirithi mikoba ya Barbara Gonzalez aliyeondoka ndani ya Simba SC kipindi hicho.

Kajula anaondoka ndani ya Simba SC akishinda kombe la Muungano 2024 pamoja na Ngao ya Jamii msimu 2023-24,kufika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika 2023-24 pamoja na kuanzisha mifumo bora ya Wanachama kama Simba Executive Network kwa ajili ya kuiongezea mapato ndani ya klabu hiyo.
Umesahau na kibegi.
 
Babra aneshaeleza, anashangaa waandishi kuandika habari za yeye kurudi Simba bila kumhusisha.
Na wewe unapita kulekule.
 
Back
Top Bottom