Imani, Miujiza na Upendo, hivi majini ya kiswahili yataelewa kiingereza?

Kuna bwana mmoja alikua anajini linaitwa John. Linapiga kingereza mbayaa.. nilikua nishazoea ya Congo yanayoongea kilingala na siku hiyo nilishangaa
 
Duh, kazi ipo.
 
Haijalishi pepo limeongea lugha gani, sisi ni kusema kimyaaaa.....in gwajiman voice.
 
jombaa majini ya kibongo yana digirii
 
Sio kwamba naikosoa imani yangu na ikihesabika hivyo naomba nisamehewe.

Hii hali ya kutoa na kukemea mapepo naona kama imekaa kimaskini maskini, mapepo yamekua yakitolewa na kukemewa tokea miaka ya 70 huko mpaka leo ni toka toka toka tuu, hivi hayo mapepo hayaoni kwamba hawatakiwi yanaendelea kuwa king'ang'anizi tu, au yanapata cha nini mno kiasi cha kustahimili fedheha wanayokutana nayo kutoka kwa manabii wachungaji na mitume?

Mimi nadhani tatizo letu sio mapepo bali mfumo wa mtazamo na akili na umaskini na haswa umaskini iwe umaskini wa akili au mali ndio msingi wa matatizo yote, hao watumishi wa Mungu wange dili na ufunguzi wa fahamu kwa waumini wao kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu hiyo miaka ya 70 hayo mapepo yapo kwa mtu huyohuyo mmoja au watu tofauti tofauti ili tujue kama toka toka inafaa au haifai...?jibu lako lizingatie kwamba sasa ni miaka 51 imepita
 
Tangu hiyo miaka ya 70 hayo mapepo yapo kwa mtu huyohuyo mmoja au watu tofauti tofauti ili tujue kama toka toka inafaa au haifai...?jibu lako lizingatie kwamba sasa ni miaka 51 imepita
Nimezungumzia tokea hizi harakati za utoaji mapepo nchi hapa kuanza nime kisia walao miaka ya 70 enzi za wakina kulipa nk.

Hayo mapepo ndio hayatolewi kwa mmoja pekee, lakini tuseme kanisa la kiuokovu labda kanisa A na labda B kila mmoja kanisa ni kwake kila kutaniko ni kukemea pepo na kuyatoa , jana hivyo hivyo, leo na kadhalika kesho, lakini hii ilianzia juzi na juzi yake!
Ndio nikajiuliza hayo mapepo hayaoni aibu kila leo ni kufukuzwa tu kwa nini yasiondoke moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapepo mengi yanafuata mfumo wa chama tawala hayana aibu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…