Imani na Mifano tata

kevoomarcus

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
495
Reaction score
905
Naam, kama ilivyo katika maisha ya kawaida, kila kitu huwa na pande mbili zinazokinzana, kama vile mrefu na mfupi, mweupe na mweusi, na kadhalika. Vivyo hivyo, imani ina pande mbili: kuamini au kutokuamini, ukweli au uongo. Mfano, unaweza kuamini timu yako itashinda mechi kesho kwa vile ina kikosi kizuri, lakini inaweza isishinde. Vilevile, kwenye imani kuhusu Mungu, anaweza kuwa yupo au hayupo.

Neno lenyewe "imani" linajieleza kwamba ni kuwa na uhakika na kitu au vitu ambavyo huna uhakika navyo. Lakini, utawakuta wafia dini (theist) wanavyotoa matusi, vitisho, na hofu kwa maneno ya kistaarabu kabisa kwa wale wasioamini Mungu. Wenye imani ya kutokuamini (atheist) hutoa hoja nzuri sana, ila wafia dini hutoa hoja kupitia maandiko na wakishindwa huanza kuleta vitisho kama vile "pumzi inakupa kiburi," "ngoja ufe ndo uone cha moto," "jehanamu inakuhusu," kama vile wameshawahi kushuhudia mambo hayo au wameshawahi kufa na kurudi.

Nilianza kuona mambo ya kiimani ni miyeyusho pale dini kuu mbili zenye wafuasi wengi duniani zilipocontradict. Uislam unasema uislam ndio dini ya haki ya Mwenyezi Mungu na Mtume Muhammad ndio njia ya peponi, huku Ukristo ukisema Yesu ndio njia bila kumkiri na kumpokea huwezi kuona mbingu. Hapo ndipo nilipojua dini ni utumwa wa kifikra ulioletwa na wageni wazungu na waarabu.

Imani nayo ni utumwa kabisa. Kuna mtu anaomba sana na kumtegemea Mungu atamsaidia lakini hajapata msaada, huku mwingine anaishi tu na maisha yanaenda. Mungu mwenye huruma na upendo hakuwa na haja ya kuumba watu wenye mapungufu ya maumbile, alikuwa anaweza kuumba watu wote wakiwa na viungo vyote kamili. Lakini imani itakwambia kuwa ni majaribu. Sidhani kama kuna mzazi ataweza kumpa jambo baya mwanae kwa kumjaribu.

Imani ni vitu vya kujifariji na kujipa matumaini yasiyo na maana. Mpaka maandiko yenyewe yanajifunga. Mfano, "utakula kwa jasho," wakati kuna watu wamezaliwa familia za kitajiri au kifalme kabisa, sijui kama nao wanasota kupata mlo. "Kuzaa kwa uchungu," kuna watu hawazai kwa uchungu bali wanazaa kwa upasuaji tena na ganzi juu.

Kuna jibu fulani wafia dini hupenda kulitoa pindi mtu akisema hakuna Mungu. Hujibu, "Nani aliumba ulimwengu, jua, binadamu, na wanyama?" Wenye kutokuamini (atheist) nao huuliza, "Nani alimuumba huyo Mungu? Kama yupo tangu milele na milele, kwanini ulimwengu usiwe ndio upo tangu milele na hakuna aliyeuumba kama hakuna aliyemuumba Mungu?"
 
Kila mtu aamini anachokiamini...nahisi itakuwa bora zaidi kuishi maisha ya amani duniani
 
Dini zilikuja kuchukua watumwa na Resourses huku Afrika !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…