kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,940
- 7,849
Katika historia ya ulaya enzi ya utawala wa Roma ukristo ulienea na kuweza kua na nguvu kubwa kwenye maisha ya watu. Sheria za kanisa zikawa na nguvu kwenye utawala na wafalme au watawala wasingeweza kuongoza bila kukubaliwa na kanisa. Ukristo ukawa na nguvu hadi kupeleka jeshi mashariki ya kati kupambania ukristo wakiita vita vya msalaba.
Baadae kabla ya kina Karl Marx na frederick Angels wakatokea wasomi kupinga kanisa na imani ya dini kwa ujumla kwa hoja. Kwamba imani ya dini inawafubaisha watu kupata majibu ya matatizo yao ya kiuchumi na kijamii ulimwenguni kwa ahadi ya kukubali mateso na kutii tawala kandamizi kwa kutegemea malipo ya kwenda mbinguni baada ya kufa.
Chambuzi za kisayansi za waandishi kama Karl Marx zilionyesha kwamba misingi ya imani kwenye dini ya kiyahudi na kikristo imejaa uongo na njonzi kwenye mafunzo yao. Walitokea wafuasi wengi kutoka tabaka la wasomi na wafanyakazi kuunga mkono na hata mabepari mwanzo waliunga mkono mapambano dhini ya imani ya dini.
Jambo ninalotaka kulionesha hapa ni kwamba mabepari na watawala haraka waligundua kupiga vita imani ya dini ni hatari kwao. Dini ya kikristo iliwataka watu kutii utawala na pia kuwatii wakubwa wote kwani wapo kwa mapenzi ya mungu. Pia iliahidi maisha mema ya peponi mbinguni kwa tabu na shida mtu atapata hapa duniani.
Kwa hivyo mabepari wa mashamba na watawala wakashikamana kufanya kazi na kanisa kuwalewesha watu na kasumba ya maisha mema mbinguni kwa tabu na mateso na dhuluma ya maisha ya duniani. Karl Marx aliita dini 'opium of society' yaani bangi ya jamii.
Katika historia ya ukoloni tunasoma mamisionari Livingstone, henri stanley na wengine wakitangulizwa kabla ya askari kuja kukamata nchi zetu.
Leo hii mnaona makanisa kibao mapya kuacha yale ya jadi. Tusiwe wajinga eti hatujui yanatoka wapi. Wakoloni mamboleo wanataka tuendelee kutafuta ufalme wa mbinguni wakati wao wanaunda ufalme wa duniani. Ukiweza kutembea miji mbalimbali duniani leo utakuta vipaza sauti vyenye kufanana kote duniani kwenye mikusanyiko ya watu kama vituo vya mabasi vikihubiria watu ufalme wa mbinguni.
Je, si ni mtu mmoja au mamlaka moja inafadhili kotei huko? Je unafikiri ni kwa ustawi mwema kwa waafrika au ni kuwafubaza kutafuta ufalme mwema kiuchumi duniani?