Mkuu .. Binafsi naamini kuna tafsiri mbili unapoongea kuhusu dini au imani.
1. Kuna wale wanaotumia dini kukinga mabaya yao na kwa maslahi yao binafsi na si vile Mungu anavyotaka. Wanatumia maandiko kupotosha nia njema ya imani na uhusiano na Mungu. Hapa namaanisha wale wanaopiga kelele kwa sauti kubwa kutumia kigezo cha dini (Kikiristu, Islam, Budha etc) lakini giza likiingia wanageuka kuwa simba wakali na wako tayali kuua hata wenzao wenye imani sawa na wao.
2. Kuna wale ambao wako kimya, Wana imani ya juu ya kile wanachoamini hadi wanakubali kuwa Mungu ni wa upendo na Amani. Aina ya watu hawa hawajali binadamu mwenzake ana dini gani ili mradi kama huyo mwenzake anayo amani na upendo na anamtukuza na kumtii Mungu kwa vile anavyoamini na siyo kinafiki. Mara nyingi watu kama hawa hawajali mwenza/mke wake ni wa dini gani. Imani imempeleka mbali zaidi na anaamini yeyote anayeamini Mungu wa kweli na kutii sheria zake basi ni mmoja wake bila kujali dini au dhehebu.
Swala la kuchanganya dini katika familia yako utaamua wewe mwenyewe kutokana na uko kwenye kundi gani la hapo juu, ingawa kama utakuwa kundi la pili unaweza kupata kipingamizi toka kwa baadhi ya mafundisho ya baadhi za dini na changamoto na jamii inayokuzunguka. Lakini mwisho wa yote.. Kitakacho kuweka karibu na Mola ni matendo yako kwa mwenzako na siyo kelele na unafiki wa hapa duniani.