Uchaguzi 2020 Imani yangu kwa Rais Magufuli hiyo kesho tarehe 28/10/2020

Uchaguzi 2020 Imani yangu kwa Rais Magufuli hiyo kesho tarehe 28/10/2020

Joined
Nov 16, 2016
Posts
30
Reaction score
52
Licha ya kwamba Rais Magufuli hajafanya vizuri katika suala la ajira ila binafsi bado nna Imani naye kuelekea tarehe 28/10/2020 hivyo anastahili kupewa miaka mitano tena katika utawala wake.

Kafanya mengi mazuri yakujivunia ukilinganisha na suala zima la uhaba wa ajira nchini.

Ni ukweli usiopingika kwamba nchi yoyote inayohitaji kupiga maendeleo kiuchumi ni lazima kuwe na kundi linaloumia hasa hasa kundi la tunaotafuta ajira rejea sula zima la mapinduzi ya viwanda barani Ulaya katika karne ya 18 mpaka 19 ni wazi kwamba watu wengi walipoteza ajira zao hivyo sina shaka kabisa na Rais Magufuli katika suala zima la uhaba wa ajira.

Ununuzi wa ndege ni kitu cha kujivunia kama Taifa kwani kumesaidia nchi yetu nayo kuwa na NATIONAL CARRIER kwani hii itaturahisishia kuitangaza nchi yetu kimataifa na kupunguza muda wa wasafiri kukaa angani kwani hakutokuwa na ulazima wa ndege zetu kuwa na destination nyingi ambapo tunaweza amua tuwe na direct flight either kutoka Marekani/ulaya kuja moja kwa moja nyumbani Tanzania bila kupitia cairo , south Africa then turudi Nairobi ndo tuingie KIA/JNIA.

Uboreshaji wa miundombinu hili ni jambo la muhimu Zaidi na la kwanza ili kuyafikia maendeleo. huwezi kupata maendele iwapo una miundombinu mibovu kwani hii itakwamisha muingiliano wa wazarishaji mali na usafirishaji wa bidhaa ama malighafi naikumbuka form one kipindi tunaandika nshu za poor infrastructure. Hivyo ninamupongeza kwa kujenga viwanja vya ndege, barabara, fly overs, kufufua reli na kuanza kwa safari za treni bila kusahau ujenzi wa meli na vivuko mbali mbali nchini.

Rais wetu umeboresha shule kongwe na kukarabati hospital za wilaya pamoja na kuanzisha vituo vya afya na zahanati nchi nzima. hili limeturahisishia upatikanaji wa huduma za afya japo bado kuna watumishi wachache wanaokukwamisha kwa maslahi yao binafsi ili ionekane huduma za afya ni mbovu.

Nina mengi yakunifanya niwe na Imani na wewe ila wacha tu niishie hapa na yaliyobakia nitayamalizia hiyo kesho kwenye sanduku la kura kwa kukupa kura yangu ili niunge mkono kazi ulizofanya kwa nchi.
 
#JPM mitano tena inamuhusu.
wamikoani mkishamaliza kupiga kura anzeni kabisa kuja kusherehekea ushindi wa 95% wa JPM.
 
#JPM mitano tena inamuhusu.
wamikoani mkishamaliza kupiga kura anzeni kabisa kuja kusherehekea ushindi wa 95% wa JPM.
Nadhani wewe ni mfata mkumbo tu.
Hujui nini kimekosekana nchini kifanywe na serikali.
 
Magufuli kesho anaweka historia tena..
Miaka mitano tena ya wengi kuisoma namba..
Maendeleo kumekucha.. 💛💚💛💚💛💯
 
Binafsi sina shaka na ushindi wa wizi, vitisho na kila kitu.......ushindi huo ukishapatikana na sherehe kufanyika, wote tunarudi kulilia ajira, kulia na TRA kodi za kizushi, kulia na bei za mazao, kulia na nyingeza ya mishahara.......Mungu atusaidie.
 
Dotto James ni ndugu yako? Manake mnalingana kwa ujinga.
 
Upinzani wa kweli ulikuwa ni kipindi cha Dr Slaa 2010.
Ushindi wa Magufuli awamu hii 2020 ni Zaidi ya asilimia 95%
 
Kumuunga mkono mtu anayefanya vizuri si dhambi.
Magufuli 5 tena.
 
Thibitisha kwamba yeye ndo kawapoteza.
siku zote hatuwezi kuishi kwa matukio ya kutengenezwa.
Kama sio yeye anaetuma watu wake kuua hawa raia wasio na hatiya kwanini ata siku moja hajawahi kukemea? Si aliapa kulinda raia na mali zao?? Mwamba anauhusika wa moja kwa moja na damu za innocent people.
 
Binafsi sina shaka na ushindi wa wizi, vitisho na kila kitu.......ushindi huo ukishapatikana na sherehe kufanyika, wote tunarudi kulilia ajira, kulia na TRA kodi za kizushi, kulia na bei za mazao, kulia na nyingeza ya mishahara.......Mungu atusaidie.
Ushindi wa wizi, vitisho?. Chama cha Mbowe mna kura za kuibiwa kweli?. Chadema kinawashabiki tu sio wanachama. Chama cha mfukoni mwa mwenyekiti. Baada ya uchaguzi lazima mpoteane vizuri pale Ufipa, no ruzuku, no michango ya wabunge, patamu hapo.
 
Magufuli ndiye Rais wa Tanzania. Hakuna chama chochote cha siasa, kinachachoweza kuishinda ccm kuanzia serikali za Mitaa mpaka Urais. Poleni waotandoto za mchana.
 
Back
Top Bottom