Imani za ajabu utotoni

Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2017
Posts
1,940
Reaction score
3,834
1. Kutema mate ulipokojoa mara baada ya kukojoa.

2. Kujaza upepo mashavuni ili usionekane ulipojificha.

3. Kushika mapu... ili msifungwe (mpirani)

4. Kuchomeka jani kwenye nywele ili mwalimu asahau kuwaadhibu.

5. Kuchora msitar kwa majivu katikati ya tumbo kuanzia juu kwenda chini, ili usivimbwiwe (kama ulikula kupita kiasi)

Ongeza nyingine.
 
Ila kwa iman zile zilifanya kazi haswa
 
Kuweka wembe/nyembe golini ili wakose magoli wapige pembeni!
 
Kwa sisi wale wa jamii za kifugaji
1. Kumpigapiga ng'ombe aliyevimbiwa kwa kiatu cha mgumuu wa kushoto eti inapunguza uvimbe.
2. Ukipotelewa na mifugo wako unatema mate kwenye kiganja cha mkono na kuyapiga na mkono mwingine, yatakaporukia ndiyo direction ya wanyama wako.
3. Kukojolea fimbo yako uliyokuwa unachungia ili kuzuia mifugo wako wasiliwe na wanyama wakali kama simba nk.
 
Mtu mwenye KIGUGUMIZI unamfunikia KIKOMBE,,,KIGUGUMIZI KINAZIDI,,,,UKILA KICHWA CHA SAMAKI unakuwa na AKILI kama SAMAKI
 
Hii post nilipoiangalia haraka nilidhani Ni mshana Jr.
 
Kutema mate kiganjani na kuyachapa kwa kidole pale unapotafuta kitu kilichopotea. Kule mate yatakapoelekea basi kitu chako kipo upande huo... Watoto wa siku hizi hawajui hiyo.
 
eti ukiwashwa kwenye kiganja cha mkono utaokota au kupata hela
 
Ya kwanza mpaka leo na utu uzima najikuta automatic tu nimefanya.
Nyingine nilikuwa napindisha vdole viwili cha kati na shahada ili mdingi asahau kunibutu. Pia nilikuwa naweka njiti ya kiberiti kwenye nywele ili asahau![emoji3][emoji3]
Kweli imani ina nguvu mengine yalikuwa yanatokea kweli. Ningekuwa na iman mpaka sasa hv ningekuwa tajiri mkubwa saaana!+
 
Kukamata Kereng'ende (Helicopter)Kisha Kuua then Kumsaga Halafu Unatakiwa Usubiri Mtoto Wa Kike Mzuriii Akojoe Kisha unamwagia Huo Unga Eti Mtoto wa Kike Atakupenda!Shida Ilikuwa Kupata Sehemu Aliyokojoa Mtoto wa Kike[emoji16][emoji16][emoji16]
Hii ya kereng'ende (dragon fly) imenikumbusha mbaaali sana. Enzi hizo tiliamini kuwa jivu la mdudu huyo mjanja sana kwa kuruka mielekeo tofauti, ukilipaka kwenye fimbo na ukamchapa nayo kabint ukapendako, basi imemaliza mchezo.
Basi bwana... Baada ya jitihada zangu za siku kadhaa nilifanikiwa kumnasa kereng'ende wangu mwenye mbawa nyekundu(iliaminika kuwa aina hii ndo the best)
Nikatafuta kifimbo changu kizuri cha mpera nikakipaka jivu la kereng'ende. Nikakificha chini ya mto wa kitanda changu ambacho kilikuwa hakijatandikwa, nikivuta muda magharibi ifike nikatimize azma yangu kwa kibint fulani kizuuri, nilichokuwa nakitamani sana(kwa sasa ni marehemu.
Kumbe huku nyuma dada yangu aliamua kukitandika kile kitanda, na alipoona kile kifimbo hakujua ni cha nini akakichanganya kwenye kuni kikala moto. Basi nilipo rudi kuchukua amali yangu bwana,sikuipata.acha nizue timbwili... Fimbo yangu... Fimbo yangu.
But kilichofuatia hapo ndo kilikuwa very interesting
Nikajua nguvu ya imani ipoje. Ukipenda kujua whats next... Kilichofuatia basi niulize.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji24][emoji24][emoji24]utoto ni ufala Sana Mzee
 
Malzia mkuu
 
Kama umechelewa shule na hutaki mwl akupige unachomeka vijiti kichwani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] eti hakuoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…