Imani za Kiswahili/Kijadi kuhusiana na ndege Kasuku

Imani za Kiswahili/Kijadi kuhusiana na ndege Kasuku

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Tunafaham mila na desturi zetu wakati flani ziliwapa majina mabaya aina flani ya wanyama, wadudu, ndege, samaki hata mimea.

Bundi anaonekana ni ndege asiyefaa kabisa mwenye mikosi na kila aina ya ubaya ambayo ameambatanishwa navyo. Mimi nlinunua bundi mwaka 2005 nifuge home. Ndugu na jamaa walinipiga vita sana na kusema hawatokanyaga kwangu. Nikamwachilia huru. Mpaka leo huwa namkumbuka sana bundi wangu.

Sasa nimetamani kufuga Kasuku. Imekuwa issue. Mwenzangu hataki kabisa kusikia habari hizo. Anasema Kasuki naye ana mambo ya kiswahili. Sasa najiuliza mambo gani. Anasema hataki hapa home nifuge kasuku. Wana mikosi sijui na nini.

Sisi wengine tunapenda sana kuwa huru. Ila jamii inayotuzunguka ina mambo mengi mpaka sasa inakuwa kero. Tunakosa Uhuru kabisa. Mpaka natamani niwe single tu niiishi maisha yangu. JE KASUKU ANA TATIZO GANI? MAANA MIASHOKI MLISEMA INALETA UGOMVI KWENYE NYUMBA. WATU WAMEKATA NOWDAYS.
 
Kuna mtu anaweza nifafanulia kasuku ana mambo gani ya kiswahili
 
Back
Top Bottom