Imebaki masaa machache sana wajisahaulishe kuwa twapaswa kuanza awamu ya sita na sio kuendeleza awamu ya tano

Imebaki masaa machache sana wajisahaulishe kuwa twapaswa kuanza awamu ya sita na sio kuendeleza awamu ya tano

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Kiutawala hapa Tanzania awamu za uongozi humaanisha muda anaokaa madarakani Rais. JPM awamu yake imekuwa ya miaka kama mitano na ushe hivi. Mwinyi, Mkpa na Kikwete awamu zao zilikuwa ni miaka kumi kumi hivi.

Nyerere awamu yake ilichukua zaidi ya miaka 20. Mama Samia awamu yake inaweza ikawa ya miaka 9unusu hivi kama akifanya vizuri.

Ili Rais wetu mama Samia aweze kufanya vizuri ni muhimu aanze kujitambua mapema kuwa amebeba awamu yake ya sita ni sio kuwa anaendeleza awamu ya 5. Anatakiwa mapema sana ajipambanue kama alivyofanya JPM.

Pamoja na JPM kujaribu kuitofautisha awamu yake na za watangulizi wake alitia dosari utofauti huo kwa kuanza kwa maneno yake kuponda mambo yaliyofanywa na watangulizi wake - ilifikia hadi kuashiria kuwa awamu ya nne ilikuwa ya majizi, akijisahaua kuwa naye kwenye hiyo awamu alikuwemo kama kiongozi.

Kwa sasa Mawaziri wanatoa maelekezo kwa watendaji wao na kuanzia jumamosi kesho tayari mambo yanaendelea kufanyika kana kwamba Samia anafanya yale yaliyopangwa na awamu ya tano. Wanataka kumfanya Mhe. Mama Samia aamini kuwa hii ni awamu ya tano kumbe sio. Wanamfanya asiamua kupanga Timu yake upya.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aligoma kata kata kuongeza mishahara ya wafanyakazi hata 0.5% tu akidai kuwa Mkubwa wake amempa hayo maelekezo kuwa mwaka 2021/22 hakuna ongezeko. Ukweli hakuna hata punguzo la kodi kwa mishahara kama mwaka uliopita kutokana na maelekezo ya Mkubwa, wakiamini kuwa ushindi wa mwaka 2020 utawabeba tu katika maamuzi yao ya kibabe.

Mheshimiwa Mama Samia Suluhu umeletwa na Mwenyezi Mungu Mwenyewe ili uweze kuweka suluhu - tafadhali subirisha Mpango Bajeti unaoharakishwa ili ukumbuke hata wafanyakazi wako kwa nyongeza hata 05%.

Makundi mengi yameumia sana awamu ya tano, anza kwa kulifariji hili kundi la wafanyakazi kwanza kwa kusimamisha mipango ya Mawaziri hao ambao wapo msibani huko wanatoa tu maelekezo kana kwamba awamu ya tano inaendelea. Tutofautishe awamu hizi kwani tathmini hufanyika kwa awamu na mwenye naye hiyo awamu.

Ajabu sana!
 
Awamu tunaangalia Rais ni nani... awamu maana yake ni zamu?
Kisheria awamu ina miaka 10. kila awamu moja ikiwa na mihula miwili,muhula mmoja ukiwa na miaka mitano.
awamu ya JPM haikuisha, mama samia ana inherit awamu ya JPM ambayo ya tano, kumalizia vipindi vyake. japo ni Rais wa sita.
kwenye awamu hatuangalii Rais.
 
Mkuu kwa mujibu wa katiba yetu awamu ni miaka kumi yenye mihula miwili ya miaka mitano mitano. Kwa hiyo mama Samia ni Rais wa awamu ya 5.
 
kisheria awamu ina miaka 10. kila awamu moja ikiwa na mihula miwili,muhula mmoja ukiwa na miaka mitano.
awamu ya JPm haikuisha, mama samia ana inherit awamu ya jpm ambayo ya tano, kumalizia vipindi vyake. japo ni rais wa sita.
kwenye awamu hatuangalii rais.
Sheria ipi?
 
Mkuu kwa mujibu wa katiba yetu awamu ni miaka kumi yenye mihula miwili ya miaka mitano mitano. Kwa hiyo mama Samia ni Rais wa awamu ya 5.
Umewafundisha watu kuwa na utaratibu wa kusoma katiba kabla hawajachangia. Tuwe na utaratibu wa kusoma katiba
 
Hii ni awamu ya tano Rais wa sita. Awamu ya sita bado mpaka uchaguzi mkuu ujao. Awamu huingia madarakani kwa uchaguzi na endapo aliyepita atashinda basi ataendeleza awamu yake.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom