Nimewapigia simu leo hii ikapokelewa na mdada fulani. Issue ni kwamba kama naweza kupata sim card ambayo inaweza ku-fit kwenye simu ya Samsung Galaxy SIII. Akaniambia kuwa wanatoa kama promotion ila lazima ninunue simu toka kwao. Sasa nikawaambia kama wanatoa kama promotion si waniuzie mimi kwa kuwa sijanunua simu toka kwao? Akaniambia kuwa kuna watu wanakata hizo line mjini niwatafute. So, nikawaambia kwa nini nisumbuke kuwatafuta na hali ninyi mna uwezo wa kunitengenezea line hiyo na mnapata mteja? Akanikatia simu. So, ngoja niende TiGo naona wanatangaza hizo sim card.