Imefika wakati serikali iangalie mishahara ya watumishi wa "Local government" maana hali zao za mishahara ni ngumu na mbovu sana

Umenena vizuri. Alafu ndio wanalalamikiwa sana, tuna demand delivery kubwa sana kutoka kwao, lakini ni watu wanaodhulumiwa. OR-TAMISEMI ni majanga. Kuna kipindi walitaka kuboresha, nadhani siasa tu. Ikaishia hewani.
 
Mishahara karibu serikalini kote ni midogo... haitoshi. Serikali yetu ina bajeti ndogo sana kulinganisha na idadi ya raia wake. Bajeti ya trilioni 44 kwa watu milioni 61 huku ukiwa na miradi inayohitaji matrilioni inakuwa ngumu mno kushughulikia hiyo ishu ya mishahara. Mimi nashauri serikali iongeze vyanzo vya mapato huku ikiondoa matumizi yasiyo ya lazima na fedha zielekezwe kwa watumishi wake. Angalau mwalimu wa shule ya msingi akianzia na mshahara wa milioni moja itapendeza.
 
Issue siyo ukubwa wa mishahara.

Tatizo kubwa ni INEQUALITY ya mishahara iliyopo.
 
Nachomaanisha "Usawa wa mishahara"

Kama kuumia WAUMIE WOTEE
Kama ni kuneemeka WANEEMEKE WOTE.

#YNWA
 

Ila ukiangalia vizuri, halmashauri ndio ina hudumia wateja wengi kuliko ofisi zoteee.

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…