Imefikia mahali kunywa juice za dukani ni hatarishi kwa afya yako kuliko kunywa soda!

Imefikia mahali kunywa juice za dukani ni hatarishi kwa afya yako kuliko kunywa soda!

Watu wangi hatutambui kwamba tatizo kubwa la kunywa soda kama Pepsi, Coca Cola nk, ni kwamba zina sukari nyingi sana ambayo si jambo zuri kwa afya yako.

Sasa utakuta watu wengi sana wamekuwa na mawazo kwamba ni vema kunywa juice za dukani (processed juice) kuliko kunywa soda, na hata wengine wakiwa tayari kuwapa watoto wao wadogo juice za dukani huku wakizuia kabisa kuwapa soda.

Huko ni kufikiri kuliko potoka sana!

Imefikia mahali ambapo kunywa juice za dukani ni hatari zaidi kuliko soda, hasa ukizingatia hizi juice zinavyotengenezwa. Navyojua ni kwamba, ukilinganisha na soda, juice ziko juu sana katika viwango vya benzene na ascobic acid, vitu hatarishi kwa afya vinavyoleta kansa, ambavyo sio tatizo katika soda!

Kumbuka kwamba, japo kuna tatizo la sukari nyingi katika soda, standard ya soda kama Pepsi au Coca Cola, inadhibitiwa kimataifa. Soda unayokunywa Tanzania inatakiwa kuwa ya kiwango kile kile kama ile utakayokunywa USA au Ulaya. Na tunajua wenzetu wako strict sana kwenye masuala ya viwango.

Tofauti na soda, juice utengenezaji wake ni local - ni kama kila mwenye kiwanda cha juice anaamua aweke madudu gani kwenye juice yake, na usimamizi wa udhibiti wa utengenezaji juice hapa nchini ni dhaifu sana. Inasemekana kuna wakati hata suala la kupitisha standard za juice nchini linafanyika kisiasa, kwa amri kutoka juu - mpeni lebel ya standard huyo - labda tu kwa sababu ni mchangiaji sana wa fedha za chama fulani. Na pia, imethibitika kwamba katika juice nyingi zilizoko madukani, viwango vya kemikali zilizowekwa si sawa na ilivyoandikwa kwenye chupa ya juice.

Na pia tukumbuke kwamba juice zimetengenezwa kukaa hata zaidi ya miaka miwili zikiwa hazijanywewa, wakati mzunguko wa soda ni mdogo sana - ndani ya mwezi mmoja soda zilizotengenezwa zinakuwa zimeisha, na hivyo sio rahisi kuwa na mabadiliko ya kikemia kama ilivyo kwa juice!

Hivyo ndugu zangu, tafakari sana juu ya soda Vs juice. Ni kweli soda zina tatizo la sukari nyingi - lakini juice matatizo yake ni sukari nyingi pia na madawa kibao yanawekwa bila udhibiti thabiti, hasa katika nchi zetu hizi. Juice nzuri ya wewe kunywa ni ya kutengeneza mwenyewe nyumbani ukitumia matunda fresh!

Kwa mnaoweza kumfikia Prof. Janabi, muulizeni swali la moja kwa moja; kama hapa Tanzania ungelazimika kuchagua kati ya juice ya dukani na soda ili unywe, ungeona angalau uko salama kunywa nini kati ya hivi vitu viwili?
Coke ya Tz haiwezi kuwa sawa na ya NY, sisi hatusimamii viwango vya ubora kuanzia kifungashio, maji na vichanganywa(ingredients) kwani hata vilivyokwisha muda wa matumizi hutumika.
 
Nakumbuka mwaka 2015 pale cocobeach Coca-Cola walikuwa wanagawa vinywaji vyao vya coka vilivyokaribia kuexpire vilikuwa vile vichupa vidogo (Bambucha) aisee nilikunywa hadi yule jamaa aliyekua anagawa akanishngaa na ilikua ukimaliza unaenda kujichukulia mwenyewe hakuna anaekuzuia
 
Hebu ona hii, halafu fikiria unakunywa kwa sababu unaamini ni pure juice kama wanavosema!

View attachment 3238333
Natural juice ni ya kuitengeneza wewe mwenyewe ,hizi za kuuziwa ni JAU....Nakumbuka zamani kulikuwa na SUper Deep yaani Pakti moja ya gram 50 unatoa juice PIPA MOJA na ina sukari ya kufa mtu.
 
Nakumbuka mwaka 2015 pale cocobeach Coca-Cola walikuwa wanagawa vinywaji vyao vya coka vilivyokaribia kuexpire vilikuwa vile vichupa vidogo (Bambucha) aisee nilikunywa hadi yule jamaa aliyekua anagawa akanishngaa na ilikua ukimaliza unaenda kujichulilia mwenyewe hakuna anaekuzuia
Una Changamoto Nyingi Sana Ila Kwa Kuanzia Tu Deal Sna Na Ghorofa Na Ela.
 
Hebu ona hii, halafu fikiria unakunywa kwa sababu unaamini ni pure juice kama wanavosema!

View attachment 3238333
Additives kibao, kuanzia rangi, ladha na sukari. Kwenye ladha huwekwa ladha ya tunda husika mf. embe, ukwaji, chungwa nk. Rangi huwekwa kutegemea na aina ya tunda lengwa. Shangaa juice nyingi za matunda aina ya embe zinaingizwa nchini toka huko Dubai na bei yake ni karibu sawa na bure. Tafakati na uchukue hatua.
 
Acha tunywe tu maisha yenyewe mafupi hayaelewek hutokunywa hizo soda sijui juice ila utajakufa Kwa ajali au magonjwa mengine kabisaaa Bora tunywee tu
 
Kuna nchi wanapaswa kunywa juice za viwandani kwasababu upatikanaji wa Matunda ni gharama sana(Mfano Kuna nchi parachichi tena lile dogo ni 12,000+ ukiweka kwenye dhamani ya Tsh...

Ila hapa bongo Parachichi unapata hadi mia tatu Embe mia mbili Mananasi hadi miatano. Hivi kwanini utengenezewe juice na kiwanda badala ya kutengeneza mwenyewe?.
 
Back
Top Bottom