Kwa udadisi na kautafiti kangu ka muda mfupi nimekuja kufahamu kwamba,Mameneja wa muziki wa kizazi kipya wanaokamata kwa sasa ni watatu tu,yaani Sallam anayejiita Mendez,Said Fella na Babutale.
Na kingine ni kwamba hawa jamaa wote ni wa kutoka mkoa wa Morogoro aidha kwa asili au makazi na kikubwa ni kwamba wamelishika gemu kiasi ni vigumu kuwasikia mameneja wa mikoa mingine iwe Mwanza,Arusha kigoma,Tanga nk kutamba juu ya hawa jamaa,kikubwa zaidi ni wao au mmoja kati ya wao anaye mmanage mwanamuziki mkubwa au kikundi cha muziki chenye jina hapa Bongo, kwa kifupi ukitaka kuwa na jina au kutoka kimuziki kuwa kwenye chama la hawa jamaa.
Swali langu kwa wengine kwenye industry hii ya Bongo fleva,ni lini na nyie mtakuja iwe kwa umoja wenu au kwa mtu mmoja mmoja kuja kuvunja ubabe huu wa hawa Moro United super Impresarios?