Imekaaje Hii,Fella,Sallam,Babutale ni wao tuu?

Makuta

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2014
Posts
924
Reaction score
959
Kwa udadisi na kautafiti kangu ka muda mfupi nimekuja kufahamu kwamba,Mameneja wa muziki wa kizazi kipya wanaokamata kwa sasa ni watatu tu,yaani Sallam anayejiita Mendez,Said Fella na Babutale.

Na kingine ni kwamba hawa jamaa wote ni wa kutoka mkoa wa Morogoro aidha kwa asili au makazi na kikubwa ni kwamba wamelishika gemu kiasi ni vigumu kuwasikia mameneja wa mikoa mingine iwe Mwanza,Arusha kigoma,Tanga nk kutamba juu ya hawa jamaa,kikubwa zaidi ni wao au mmoja kati ya wao anaye mmanage mwanamuziki mkubwa au kikundi cha muziki chenye jina hapa Bongo, kwa kifupi ukitaka kuwa na jina au kutoka kimuziki kuwa kwenye chama la hawa jamaa.

Swali langu kwa wengine kwenye industry hii ya Bongo fleva,ni lini na nyie mtakuja iwe kwa umoja wenu au kwa mtu mmoja mmoja kuja kuvunja ubabe huu wa hawa Moro United super Impresarios?
 
Hao mameneja wengine hawana mbinu za kushindana na hao,ila wanachokifanya ni kujaribu kuwashusha wasanii wanaowasimamaia hao (wakina tale) wakiamini kwamba wale wasanii wakishuka na wao ndio watatamba. Na hiyo mbinu wamewaambukiza hadi wasanii wao kwa kuwaminishwa kuwa wao hawataweza bila ya DIAMOND PLATNUMZ kushushwa kwanza.
 
Hao huwa ni mameneja au walinzi wa diamond? Maana Kila picha wakitupia wako Pembeni yake, nna shaka mpaka toilet huwa wanamsubiri mlangoni
 
Kwa udadisi na kautafiti kangu ka muda mfupi nimekuja kufahamu kwamba,Mameneja wa muziki wa kizazi kipya wanaokamata kwa sasa ni watatu tu,yaani Sallam anayejiita Mendez,Said Fella na Babutale.

Na kingine ni kwamba hawa jamaa wote ni wa kutoka mkoa wa Morogoro aidha kwa asili au makazi na kikubwa ni kwamba wamelishika gemu kiasi ni vigumu kuwasikia mameneja wa mikoa mingine iwe Mwanza,Arusha kigoma,Tanga nk kutamba juu ya hawa jamaa,kikubwa zaidi ni wao au mmoja kati ya wao anaye mmanage mwanamuziki mkubwa au kikundi cha muziki chenye jina hapa Bongo, kwa kifupi ukitaka kuwa na jina au kutoka kimuziki kuwa kwenye chama la hawa jamaa.

Swali langu kwa wengine kwenye industry hii ya Bongo fleva,ni lini na nyie mtakuja iwe kwa umoja wenu au kwa mtu mmoja mmoja kuja kuvunja ubabe huu wa hawa Moro United super Impresarios?
Wanajua kucheza na vyombo vya habari na wameviteka..
 
Ndo nataka kujua hivi hakuna wengine waliopo kwenye industry hii ya muziki wakajitokeza na mbinu mbadala ya kuja na kuibua vipaji vingine na pia kuleta ushindani kwa mameneja hawa waliopo? mbona kwenye music video tunaona kuna madirector wapya wengi tu na wanaleta ushindani wa nguvu kwa wakongwe?
 
Niorodheshee wasanii waliotolewa na kila mmoja ili niona kama kweli wasanii wote waliotoka wamepitia mikononi mwao
 
Back
Top Bottom