Imekaaje hii Kisheria?

Imekaaje hii Kisheria?

George Betram

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
4,672
Reaction score
6,272
Nimepita sehemu nimekuta jamaa katolewa vyombo na mama mwenye nyumba. Jamaa amekuta vitu vimenyeshewa na mvua.
Wanasheria, imekaaje hii?
 
Sasa kama ameshindwa kulipa kodi na huenda kaleta jeuri. Unataka mwenye nyumba afanyaje? Nyumba nijenge mwenyewe kwa pesa zangu harafu uniletee jeuri. Tambua baba mwenye nyumba ana akili timamu hawezi kutoa vitu nje tu bila mfarakano na mpangaji.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Kabla ya mwenye nyumba kutoa vyombo kuna taratibu anatakiwa atumie ikiwemo kufungua kesi baraza la nyumba ila kama ametoa kienyeji itakula kwake mbali na kudaiwa uharibu wa mali anaweza kudaiwa upotevu wa mali
 
Nimepita sehemu nimekuta jamaa katolewa vyombo na mama mwenye nyumba. Jamaa amekuta vitu vimenyeshewa na mvua.
Wanasheria, imekaaje hii?
Wapi huko mvua zinanyesha mwezi huu?
 
Sasa kama ameshindwa kulipa kodi na huenda kaleta jeuri. Unataka mwenye nyumba afanyaje? Nyumba nijenge mwenyewe kwa pesa zangu harafu uniletee jeuri. Tambua baba mwenye nyumba ana akili timamu hawezi kutoa vitu nje tu bila mfarakano na mpangaji.
Sawa, hayo yote uliyouliza siyaelewi kwasababu nilikuwa mpita njia. Lakini pia nafikiri kuna utaratibu wa kumtoa mpangaji kwenye nyumba yako. Vipi kama yule mpangaji angesema kulikuwa na pesa kiasi fulani kwenye chumba chake na hizo pesa hazionekani baada ya mwenye nyumba kutoa vitu vyake?
 
Back
Top Bottom