Imekaaje Hii, miaka yote Toni Kroos anavaa viatu Aina moja TU kila mechi?

Juzi kati aliulizwa kuhusiana na jambo hilo ila alisema hivyo viatu huwa anavaa kwenye mechi maalumu na muhimu zaidi

Anaamini hiyo ni pair ya kiatu yenye bahati zaidi katika maisha yake ya soka
Kadanganya,
Huu mguu Anavaa kila mechi[emoji28]
 
Hapo usikute kashalamba pesa kwaajili ya tangazo kwa adidas
 
Una uhakika umemfatilia au umeona sehemu hii hbr nawe ndio ukaileta hp? Dunia ipo kiganjani hii!
 
Jamaa anavaa viatu ambavyo Adidas waliacha kutengeneza.

Ila kwakuwa ana mkataba na Adidas jamaa wanamtengenezea viatu toleo hilo kwa ajili yake.

Hata juzi kwenye Fainal ya UCL dhidi ya Liverpool, Adidas walimletea viatu maalum kama vile anavyovaa kila siku vikiwa na maandishi ya Final Paris lakini yeye aliamua kuvaa vile alivyovaa kwenye Fainali ya World Cup 2014
 
Yeye si ni mjerumani anatangaza kampuni ya kwao ya Adidas..
 
Hana pair moja lkn ana design moja kumbuka wachezaji hawanunui ivo viatu kariakoo wanatengenezewa na kampuni huenda hiyo ndio design aliyoipenda
 
Hii ni injini ya kijerumani yenye 6 pistons! Hata ikiamua kuvaa ndala iachwe tu!
 
Ana mkatba na hao jamaa
Hujaelewa mada mkuu, issue sio kuwa na mkataba Bali issue ni kuvaa toleo la Adidas la zamani, hizo njumu unazoona ni toleo la 2014 na leo tupo 2022 na kila mwaka Adidas wanatoa matoleo mapya

Ndomana kuna baadhi ya wachingiaji wamesema anavaa hivo viatu kwenye game muhimu zaidi akiamini ni viatu vyenye bahati katika mafanikio yake ya mpira
 
Huyu ni kama mimi ila ni nje ya mada kidogo.

Mimi nilivokuwa chuo nilikuwa nakaa siti ileile kwenye hall tofauti tofauti hata iwaje. Nikiingia chumba mfano m1 basi nitakaa siti ileile hivyohivyo m2 na kuendelea sibadilishi.

Pia kipindi cha ue kuna nguo zangu nilikuwa navaa hiyo pair bila kubadilisha kitu mpka mitihani inaisha.

Afu me sionagi shida kunununua hata nguo pair tatu zinazofanana kila kitu.

Basi sijui kwa nini..
 
Umenikumbusha kitu hahahh,kipindi cha masomo na mitihani huwa nina kalamu zangu hizo,yaani siku ya Kwanza kuingia darasani hadi tunafunga shule mimi utanikuta na peni za aina moja tu, nikitumia nyingine nahisi kabisa kuna kitu kimepungua sometimes naziita kalamu zangu za bahati...
 
Kama mm Nina surual nlionunua ambayo navaa kila nkienda tongoza demu mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…