KERO Imekaaje unanunua umeme, TANESCO wanakata pesa bila kukwambia ni deni gani unakatwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
659
Reaction score
1,101
Habari wakuu.

Hili jambo la kununua umeme halafu wanakata pesa bila kukwambia ni deni gani na ni kiasi gani, kwenu limekaaje?

Nimenunua umeme wa shilingi 2,000, lakini nimepewa umeme wa shilingi 409 tu, halafu shilingi 1,500 imeandikwa debit collection.

Tuseme ni ile kodi ya majengo. Sasa kwa nini hawatumi kiasi kinachodaiwa ili siku wakikata pesa zao nijue nanunua umeme unaoendana na deni lao?

Najiuliza, ningenunua umeme wa shilingi 1,000, wangekata kiasi gani hapo?
 
Kodi ya kunenepesha majizi na mafisadi ya CCM.
 
Habari Ndugu Wateja,

Tafadhali tunaomba radhi kwa kuchelewa kuona taarifa hii na kutoa majibu kwa wakati.

Ni kweli kwamba kiasi hicho hukatwa kila mwanzo wa mwezi, na baada ya malipo kukamilika, mteja huweza kununua umeme kwa kiwango chake kama kawaida.

Tafadhali fahamu kuwa tunatoa taarifa kuhusu huduma zetu kupitia njia mbalimbali rasmi za mawasiliano.

Endapo hupokei taarifa kutoka kwetu, tunaomba ututumie namba yako ya simu pamoja na makazi yako (Wilaya na Mkoa) kupitia inbox yetu, ili tuweze kukuunganisha kwenye makundi yetu ya WhatsApp pamoja na orodha ya “Bulk Messages.” Hii itakuwezesha kupata taarifa kwa wakati, kuuliza maswali, na kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha huduma zetu.

Asanteni na karibu sana. ^HN
 
Safi sana inapendeza kwa kutoa maelezo yaliyo nyooka tanesco mnaangaza maisha
 
Back
Top Bottom