Habari Ndugu Wateja,
Tafadhali tunaomba radhi kwa kuchelewa kuona taarifa hii na kutoa majibu kwa wakati.
Ni kweli kwamba kiasi hicho hukatwa kila mwanzo wa mwezi, na baada ya malipo kukamilika, mteja huweza kununua umeme kwa kiwango chake kama kawaida.
Tafadhali fahamu kuwa tunatoa taarifa kuhusu huduma zetu kupitia njia mbalimbali rasmi za mawasiliano.
Endapo hupokei taarifa kutoka kwetu, tunaomba ututumie namba yako ya simu pamoja na makazi yako (Wilaya na Mkoa) kupitia inbox yetu, ili tuweze kukuunganisha kwenye makundi yetu ya WhatsApp pamoja na orodha ya “Bulk Messages.” Hii itakuwezesha kupata taarifa kwa wakati, kuuliza maswali, na kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha huduma zetu.
Asanteni na karibu sana. ^HN