#COVID19 Imekuwaje Kiwanda cha chanjo ya Covid-19 kijengwe Kenya ilihali ilitangazwa kingejengwa Tanzania?

#COVID19 Imekuwaje Kiwanda cha chanjo ya Covid-19 kijengwe Kenya ilihali ilitangazwa kingejengwa Tanzania?

Imekuwaje Kiwanda cha chanjo ya Covid kimepelekwa Kenya ilihali mama akiwa Ulaya alitangaza kuwa kitajengwa Tanzania. Je wajenzi walimdanganya au hakusikia vizuri?

Je, aliambiwa kitajengwa karibu na Tanzania, yeye akachukulia kuwa kitajengwa Tanzania?
Tatizo utawala wa Tanzania hauaminiki haijulikani kesho atatawala Nani anaweza kufunga hicho kiwanda nakusema ninjama za mabeberu kinazalisha virusi !!
Kumbuka enzi za mwendazake
 
Tatizo utawala wa Tanzania hauaminiki haijulikani kesho atatawala Nani anaweza kufunga hicho kiwanda nakusema ninjama za mabeberu kinazalisha virusi !!
Kumbuka enzi za mwendazake
Kingejengwa Tanzania ungekuja kuponda humu kuwa tunataka kuletewa magonjwa

Nyie hamueleweki ndo mana mnaitwa pingapinga fc Au malalamiko fc
Jibu lako haliendani na swali ninalojiuliza. Siyo lazima kuwa kiwanda khicho kijengwa Tanzania, ninachouliza mimi ni kuwa Rais alitanganza kitajengwa Tanzania, lakini sasa kimejengwa Kenya. Isingetangazwa na rais, wala usingesikia swali hili
 
Mlima Kilimanjaro uko Kenya ni sawa tu acha wajenge huko huko.

Miaka fulani Hayati Reginald Mengi (RIP) alipofiwa na mwanawe Motie kwa shida ya moyo (japo inasemekana na mengine yalikuwepo ) aliamua ajenge hospital ya moyo.

Hata foundation ilikuwa tayari, akawekewa zengwe la maana akashindwa kuendelea.

Acha wajenge hiyo ya covid huko huko tutavuka kuchanja anyway.
Zamani kulikuwa ni ukirtimba sana wizara ya afya kuhusu tiba ya magonjwa ya moyo kwa vile wizara ilikuwa inawapeleka India ambako mpaka leo hatuji Wizara ilikuwa inafaidikaje. Kuna jamaa mmoja Dr Masau alishirikiana na taasisi ya Moyo Texas kujenga hospitali ya Moyo Dar es Salaam ili kuepeusha haja ya watanzania kupelekwa India, akawekewa mkwara sana na waizara ya afaya kusudi iendelee kutoa vibali vywa kwenda India. Nadhjani ukiritimba huo uliondolewa au kupungua sana baadaye hadi kufuikia Muhimbili kuimarishwa kuwa na taasisis nzuri ya Moyo.
 
Jibu lako haliendani na swali ninalojiuliza. Siyo lazima kuwa kiwanda khicho kijengwa Tanzania, ninachouliza mimi ni kuwa Rais alitanganza kitajengwa Tanzania, lakini sasa kimejengwa Kenya. Isingetangazwa na rais, wala usingesikia swali hili
Kwani kiwanda Cha Kenya kinajengwa na kampuni iliyomwahidi Rais !!
 
Kwani kiwanda Cha Kenya kinajengwa na kampuni iliyomwahidi Rais !!
Swali lako ni zuri sana; kwa hiyo unadhani na sisi tusubiri cha kwetu bado kinakuja?

Hata hivyo ninajua kuwa Rais Biden ndiye aliyesukumiza viwanda vya Moderna na Pfizer kufungua production Africa, na vinafanya hivyo kwa kutumia hela ya walipa kodi wa marekani, siyo kuwa wanakuja kibiashara. Vikachagua South Africa, Kenya, Rwanda na Senegal. Sasa sijui mama yeye aliongea na kiwanda gani kingine labda cha China ambacho kwa sasa kina operations zake Misri na chanjo zake haziaminiki.

Ninachojua ni kwamba Tanzania tuna mambo ya kitoto mengi sana yanayosababisha tuonekane kichekesho mbele ya mataifa, ingawa wenyewe hatuoni hilo. Hii EAC itazisaidia sana nchi za Kenya na Rwanda kuliko Tanzania na DRC ambazo ndizo zina resources nyingi, na hii ni kutokana na serikali zetu kujienedsha kitoto.
 
Back
Top Bottom