ukikaidi utapigwa2
JF-Expert Member
- Feb 24, 2015
- 15,265
- 29,991
Sawa shabiki sambusaAcha ushabiki maandazi.Ule mpira wa faulo utaupunch vipi uelekeo unaoutaka? Sio kila mpira kipa anaweza kupunch uelekeo anaoutaka, akilazimisha hivyo anaweza kujifunga.
Huwezi jiuliza kwanini hata Simba sasa hivi hawana imani na Manula? ni kipa mzuri ila kwa sasa form yake imeshuka hata kwa kumuangalia tu unaona physic yake haipo sawa kingine Novatus ni mchezaji mzuri ila hivi karibuni amekua na reckless play anatakiwa kubadilikaMimi Hata simlaumu Manula ,ndiyo uwezo wake ulipoishia , Hata ingekuwa ndiyo mimi Manula nachaguliwa nisingekataa .
Wakulaumiwa ni KOCHA hajui first eleven yake Mpaka sasahivi na selection yake ni poor na amekaa na timu muda wa kutosha .
Hawa wachezaji wa nje wanacheza viwango vya chini sana huko waliko na hakuna ushindani wowote ni mambo ya kuiga tu ionekane na Tanzania imeita wachezaji wake wa nje .
Nova anaechezea Ukraine anawekwa benchi mechi za uefa .
Nafuu wachezaji wa yanga , simba na azam walio Kwenye mechi za caf champions league au caf confederation Mara kwa Mara .
KariaUnashauri nani adake badala ya Manula
Tanzania hatuna na makipa wazuri, na wanashindwa kujifunza kwa Diarra. Mwaka jana Mnatta alifanya kazi nzuri sana alipolinda lango la Yanga dhidi ya TP Mzembe huko Lubumbashi wakati Diarra akiwa nje ya nchi, lakini alipopewa tena jukumu hilo huko Algeria dhidi ya Belouizdad akaboronga. sana.Unashauri nani adake badala ya Manula
Kazi yake ni kutema na sio kutema tu ni kutemea ndani ya box na sio njeBinafsi huwa sitazami mechi za Simba SC ila baada ya kuangalia mpira wa stars leo kwakweli nimeona utofauti kati ya Diarra na Manula ni mbingu na ardhi!
Yaani leo nimejua ni nini maana ya kipa!. Sijazoea kabisa kuona makosa ya hovyo kiasi hiki, kipa kutema mipira ambayo alipaswa kuidaka, hususan unapocheza na wapinzani hatari kama morroco! Au huyu kipa anaumwa mikono?
Hivi mashabiki wake wamewezaje kuishi naye? Haya ni mambo ambayo mashabiki wengi hususan wa Yanga hawajazoea kabisa!
Kuna mashuti unapaswa uukumbatie mpira kwa nguvu japo inatokea mara kadhaa unatema ila unahakikisha unafanya clearance, lakini hili shati linatema mipira anayopaswa kudaka/kukumbatia.
Leo nimejua!
Hivi unafikiri kukumbatia mpira ,uliopigwa Kitaalnu ni sawa na kumkumbatia mkeo!?Binafsi huwa sitazami mechi za Simba SC ila baada ya kuangalia mpira wa stars leo kwakweli nimeona utofauti kati ya Diarra na Manula ni mbingu na ardhi!
Yaani leo nimejua ni nini maana ya kipa!. Sijazoea kabisa kuona makosa ya hovyo kiasi hiki, kipa kutema mipira ambayo alipaswa kuidaka, hususan unapocheza na wapinzani hatari kama morroco! Au huyu kipa anaumwa mikono?
Hivi mashabiki wake wamewezaje kuishi naye? Haya ni mambo ambayo mashabiki wengi hususan wa Yanga hawajazoea kabisa!
Kuna mashuti unapaswa uukumbatie mpira kwa nguvu japo inatokea mara kadhaa unatema ila unahakikisha unafanya clearance, lakini hili shati linatema mipira anayopaswa kudaka/kukumbatia.
Leo nimejua!
Mfimfiche manula kwenye kichaka cha ugonjwa,,Manula bado hanapona ni vile mpira wetu una mambo mengi
Umeangalia mechi ya Cape Verde vs Msumbiji?Angalia makipa wengine wana punch mpira pengeni sasa Manula ana punch mpira kuelekea ndani wanakuachaje?