Binafsi huwa sitazami mechi za Simba SC ila baada ya kuangalia mpira wa stars leo kwakweli nimeona utofauti kati ya Diarra na Manula ni mbingu na ardhi!
Yaani leo nimejua ni nini maana ya kipa!. Sijazoea kabisa kuona makosa ya hovyo kiasi hiki, kipa kutema mipira ambayo alipaswa kuidaka, hususan unapocheza na wapinzani hatari kama morroco! Au huyu kipa anaumwa mikono?
Hivi mashabiki wake wamewezaje kuishi naye? Haya ni mambo ambayo mashabiki wengi hususan wa Yanga hawajazoea kabisa!
Kuna mashuti unapaswa uukumbatie mpira kwa nguvu japo inatokea mara kadhaa unatema ila unahakikisha unafanya clearance, lakini hili shati linatema mipira anayopaswa kudaka/kukumbatia.
Leo nimejua!