A
Anonymous
Guest
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI imetoa malipo ya fedha za kujikimu kwa watumishi wa afya walioajiriwa kati ya Januari 2025 na Aprili 2026. Hata hivyo, walimu walioajiriwa katika kipindi hicho hicho wameachwa bila kupatiwa stahiki hizo.
Kwa kuwa fedha za kujikimu ni stahiki ya watumishi wa umma wanaokidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, tunaomba Serikali na mamlaka husika kutoa ufafanuzi kuhusu tofauti hii ya utekelezaji na kuhakikisha walimu wa ajira mpya nao wanapatiwa haki yao.
Tunasisitiza umuhimu wa usawa katika utoaji wa stahiki kwa watumishi wa sekta zote za umma, ikiwemo elimu na afya, ili kuepusha hisia za ubaguzi na kuimarisha morali ya watumishi.
Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kutenda haki kwa kuhakikisha walimu wa ajira mpya wanapatiwa fedha za kujikimu kama wenzao wa sekta ya afya, kwa kuzingatia misingi ya usawa, haki na sheria bila ubaguzi.