Imenishangaza

Imenishangaza

Lovehate

Member
Joined
Apr 26, 2018
Posts
52
Reaction score
75
Ujue sisi tunaopata amani ya moyo pale tunapokuwa tumekaa peke yetu huwa tunaongea na kujijibu wenyewe mambo mengi sana.

1. Nilijiona mpweke sana nikajiuliza inakuwaje sina hata group moja la wasap? Saa hivi ningekuwa nachati chati tu, badae naingia insta nakuta dm "kaka vipi kuna group la shule (sec) kama utapenda nikuunge"
japo nilikataa ila ilinishangaza

2. Niliachika na girl niliyempenda sana,sababu ya maana sina yeye aliyeamua kuniacha ndio anajua, sasa sijui kama nishapona au bado ila moyo unaniambia bado nampenda ila akili inaniambia hanifai tena (nipo upande wa akili)

Sasa leo kwenye kuongea peke angu nikajiuliza hivi ikitokea kaniomba msamaha na turudiane nimjibu nini? Yakaja majibu mengi ila la kurudiana halikuwepo nikaishia hapo,badae naingia wasap nakuta sms zake japo ni ujumbe usionihusu na najua pa kuufikisha.

Pia hili limenishangaza kumfikiria mtu na kuona sms zake.

*nimeshare tu unaeza sema chochote pia tu*
 
Kwa hali uliyonayo nakushauri usimfikirie wala kumuwaza virus wa COVID-19.
Maana itakua sawa na kutumia choo ndotoni.
 
Hata mimi inanitokeaga..tena mara nyingi..kuna siku nilikuwa naangalia tv..chanel ya ulaya huko..sasa katika yale matangazo tangazo..kuna tangazo likapita nahisi lilikuwa la mtandao wa simu za huko kwao..ikatokea namba ya 155# (sijui ilikuwa inahusu kujiunga na bando zao sielewei)..ikatokea karibu nusu saa nzima naiwazia ile namba...mpka natoka kwenye tv naenda mtaani kwa masela ile namba inajirudia rudia kichwani..yaan haifutiki.

Usiku wake kama saa 1 hivi Nilikuwa na buku tigopesa nikacheza Tatumzuka nikaweka zile namba 155 kwa dau la jero then nikaendelea na .mambo yangu..huwezi amini imefika kwenye saa mbili hiv ..ikaingia sms Imethibitshwa umepokea tsh 82000 toka tatu mzuka...........

Mara kidogo ikaja nyingine namba zako 155 zimelngana kwenye droo ya tatumzuka ya saa 1.....

dah...nilimaind sana kwanini nisingeweka dau la buku..

Nikaenda zangu giraffe lounge njombe hiyo...nikaagiza vitakasa koo vingi sana
 
Kuna fulana nikivaa lazima nikutane na binti fulani hivi nilisoma naye. Ikaenda mpaka siku moja nikamwambia "Nataka ujue kua nina fulana zaidi ya moja ila sielewi kwanini nikiivaa hii ndiyo tunakutana" akajibu "Twende kwako nikaone kama kweli una fulana zaidi ya moja"
 
Kuna fulana nikivaa lazima nikutane na binti fulani hivi nilisoma naye. Ikaenda mpaka siku moja nikamwambia "Nataka ujue kua nina fulana zaidi ya moja ila sielewi kwanini nikiivaa hii ndiyo tunakutana" akajibu "Twende kwako nikaone kama kweli una fulana zaidi ya moja"
Kimasiara vp?
 
Mkuu Bujibuji dhana ya telepathy inaingia kweli hapa?

Nijuavyo mimi hiyo ni non-physical na au non-human sensories communication between two or more individuals.

Sasa kama huyo anashinda tatu mzuka inahusiana vipi na telepathy?
 
wataalamu wa mambo ya kiroho wana la kuongezea hapa.

simu zetu zimekuwa zikitupa kampani,lakini kwa wakati huo huo zinatuondolea utulivu wa nafsi kuwasiliana na mzingira tunayoishi.kuna uzi humu wa jamaa mmoja anawaasa watu kukaa peke yao kwa muda flani wakiwaza mambo binafsi.

hata wataalamu,steve jobs,einstein,isaac.walikaa sehemu tulivu peke yao ndipo zikazaliwa ideas ambazo zimebadili ulimwengu kabisaa.nikasikia jobs aligoma watoto wake wasitumie ipads nk.

ukikaa peke yako unazalisha fantasy nyingi sana ambazo kama utaamua zinageuka kuwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom