Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Hii story imeniuma sana. Pole sana Mkuu. Wewe pamoja na familia yako yote mko pamoja nami katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha mjukuu Doris. ......May her soul rest in peace - Amen

Thanks sana, camera yangu iko mbali ila nitawawekea picha za Dorris kwenye mazishi!!!
 

Nashukuru ndugu, baadae nitarusha picha za mazishi ya Dorris
 
Pole sana ndugu yangu, umenikumbusha nilivoshuhudia bi mkubwa wangu akizidiwa usiku wa manane na hospitali ya AICC Arusha na manesi wakamchoma dawa ya usingizi ili asiwapigie kelele badala ya kutafuta chanzo cha mgonjwa kupiga kelele, kumbe ilikuwa malaria chronic, hakupatiwa vipimo vyovyote hapo AICC, kutokana na dawa ile waliyomchoma, alipoteza fahamu, kukaa kwenye koma wiki mbili na kufariki hospitali ya KCMC. Madaktari KCMC walidai alikuwa na malaria kali sana na shinikizo la damu. Inaniuma hadi leo na nimetokea kuichukia sana ile hospitali. Tuwe makini na hospitali za Arusha.

Yote mwachie Mungu na Time heals the pains, pole pole sana, najua unavyojisikia.

May out little angel Dorice RIP.
 

Pole sana mkuu, hii habari imenigusa sana, nasikia uchungu maana niliwahi kukutana na same issue.
 

Asante sana, AICC ndio hapafai kabisaaaaaaaaaaaaaaa, sijui hata wanafanyaga nini pale. Kifupi ni kwamba Arusha hakuna hospitali
 
Kwanza pole sanaaaa.

Pili, nenda tu kafungue mashitaka rasmi na wakichunguzwa itaonekana uzembe uliofanyika na itakuwa fundisho kwa wote. Juzi Dr amemchoma sindano jamaa yetu akafa hapohapo, sindano wala haina sababu, basi tu. Bahati yao sikuwepo na waliokuwepo waliona - kazi ya Mungu haina makosa (kama wanavyosema wao). Please dont let this pass... Anza na huyo Longdare, hao watu wana miiko yao na taratibu zao, washitaki.
 
Poleni sana mkuu! Mungu awatie nguvu na kuwapa faraja ya pekee kwa familia yote! Hakika inauma sana...poleni sana!
 

Wala usijali mkuu hata haya maelezo uliyotoa yanatosha sana hamna noma mkuu...tupo pamoja na hili swala linashughulikiwa wala usijali....zaidi sasa hivi endeleza maombezi kama kawaida....

Again pole sana....
 
Pole sana na familia yote. Thread imenitoa machozi.
May our little angel Dorris rest in peace.
 
Pole sana Blue Balaa na MUNGU muweza yote awape moyo wa uvumilivu.
Tatizo ulilokumbana nalo ni tatizo linalotukumba wengi si Arusha tu bali Tanzania nzima. imefika wakati watoa huduma wanaitoa kwa mazoea badala ya kutumia taaluma zao. hili ni tatizo la system nzima katika serikali na idara zake. lakini inapofikia hata hospitali binafsi nazo zinaingia kwenye mkumbo huo huo basi maisha yetu yapo hatarini sana.
Ndiyo maana mimi sishangai na sintashangaa kuona watu kwa maelfu wakikimbilia Loliondo kwa Babu ili kupata tiba isiyo na masharti na inayotolewa kwa moyo wa huruma na wenye kujenga matumaini mapya kwa wagonjwa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DORRIS MAHALI PEMA PEPONI, AMINA.
 
Pole sana Mkuu. Huu ni uzembe mkubwa ambao umekithiri sehemu zote za huduma za wananchi. Ni wengi sana wamefariki kutokana na uzembe wa madaktari na manesi lakini hatua zozote hazichukuliwi, ndio maana wao wanaona ni kawaida tu na kutukana watu. Tabia hii imeanzia ngazi za juu za serikali hadi kusambaa katika ngazi zote. Hii ni cancer ambayo itaangamiza taifa hatua zisipochukuliwa mapema.
 
Poleni sana, maelfu ya watoto chini ya miaka mitano wanakufa kila siku kwa uzembe wa madaktari na manesi , pneumonia hata ikiwa severe ikapata proper management at a right time watoto wanapona. Hiyo ilikuwa emergency case. Siku hizi hakuna ethics kbsa za kazi. Nimeumia sana, najua machungu yenu hasa mama Dorris. MUNGU wetu aliye hai awatie nguvu na uvumilivu. Kipenzi chetu Dorris apumzike kwa amani.
 

Saharavoice big up, umeongea maneno mazuri sana, Mungu akuzidishie hekima mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…