Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Hii story imeniuma sana. Pole sana Mkuu. Wewe pamoja na familia yako yote mko pamoja nami katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha mjukuu Doris. ......May her soul rest in peace - Amen

Thanks sana, camera yangu iko mbali ila nitawawekea picha za Dorris kwenye mazishi!!!
 
Mkuu,

Mwisho wa taarifa yako nimejikuta natoa machozi kwa sababu kuu mbili,

1. Nimemuhurumia malaika ambaye roho yake imetoweka kwa sababu tu ya uzembe wa watoa huduma.
2. Hii imenikumbusha kifo cha Mama yangu mzazi ambacho lilitokea pale muhimbili mwaka 2000 kwa uzembe wa ma nurse kwa mtindo huo huo. Pamoja na kununua dawa kama alivyoshauri daktari, manesi hawakuwa tayari kumuwekea dripu na kumpa hizo dawa kama walivyoelekezwa na daktari. Hii ilinifanya niwaambie ndugu zangu kwamba endapo nitakuwa mgonjwa ghafula na ikabidi nipelekwe hospital, basi kuliko kunipeleka kwenye hospitali yoyote ya serikali hapa Dar, basi ni bora waniache nifie ndani!!!!

Pole sana mkuu wa kumpoteza mjukuu wako kwa uzembe wa watoa huduma.

Tiba

Nashukuru ndugu, baadae nitarusha picha za mazishi ya Dorris
 
Pole sana ndugu yangu, umenikumbusha nilivoshuhudia bi mkubwa wangu akizidiwa usiku wa manane na hospitali ya AICC Arusha na manesi wakamchoma dawa ya usingizi ili asiwapigie kelele badala ya kutafuta chanzo cha mgonjwa kupiga kelele, kumbe ilikuwa malaria chronic, hakupatiwa vipimo vyovyote hapo AICC, kutokana na dawa ile waliyomchoma, alipoteza fahamu, kukaa kwenye koma wiki mbili na kufariki hospitali ya KCMC. Madaktari KCMC walidai alikuwa na malaria kali sana na shinikizo la damu. Inaniuma hadi leo na nimetokea kuichukia sana ile hospitali. Tuwe makini na hospitali za Arusha.

Yote mwachie Mungu na Time heals the pains, pole pole sana, najua unavyojisikia.

May out little angel Dorice RIP.
 
JAMANI NIPELEKE WAPI HAYA MALALAMIKO?
.
Mnamo saa saba na robo hivi usiku nilishuhudia malaika huyu (Dorris) akikata roho hodini katika hospitali ya Levolosi Arusha ambako ndio ward ya watoto wa Mt Meru ilipo. Dorris alifikishwa hospitalini hapo mnamo saa 5 kamili usiku na alipopimwa aligundulika kuwa anaumwa na Pnewmonia which also triggered her sugar mpaka kufikia 19. Alichomwa sindano, akawekewa oxygen na wauguzi wakaendelea na shughuli zao. Dorris alijatahidi sana kutetea uhai wake kwa takribani masaa mawili tukiwa mimi na mama yake (mkwe wangu) tunamkodolea macho kwani hatukuwa na la kufanya. Basi ilipotimia saa saba na robo mjukuu wangu alivuta pumpzi yake ya mwisho akiwa mikononi mwa mama yake namimi nikiwa pembeni. Hakukuwa na Nurse wala Daktari.
THE WHOLE SCENARIO:
1. Dorris alianza kuugua nyumbani mnamo majira ya saa 1 usiku na kupelekwa private hospital maeneo ya kaloleni (Arusha) inayoitwa Eben Hospital. Daktari aliyekuwepo zamu alimpima na akasema hana ugonjwa wowote. Lakini cha kushangaza akampa vichupa vitatu vya dawa alivyowatoza shs 30,000 halafu akamwambia mama yake Dorris ampeleke mtoto kwa Dr Mohamed Hospital iliyopo tank la maji. Kama hana ugonjwa kwanini ampe dawa na kum refer kwenda hospitali nyingine?
2. Mama Dorris na mototo walifika kwa Dr Mohamed majira ya saa nne usiku hivi. Walivyofika hospitalini hapo, wauguzi hawakujali kuwapokea wala kuwasikiliza isipokuwa walimwambia mama Dorris ampeleke mototo Mt Meru Hospital kwasababu wao wana wangonjwa wengi sana. Mama Dorris aliondoka na mototo wake kuelekea Mt Meru Hospital.
3. Walifika Mt Meru Hospital mnamo saa nne na nusu na kupokelewa na Dr Longdare ambaye ndio alikuwa Daktari wa zamu. Dr Longdare hakuwapatia huduma yoyote zidi ya kumwambia mama Dorris kwamba idara ya watoto imehamishiwa Levolosi hivyo ammpeleke mototo huko. Mama Dorris ndo akanipigia simu na tukakutana Levolosi. N.B. Baba yake Dorris ni mototo wangu anaefanya kazi mbuga za wanyama hivyo siku hiyo alikuwa mbugani.

MALALAMIKO
1. Kwanini Daktari wa Eben akasema Dorris hana matatizo yoyote na kisha kum refer kwenye hospitali nyingine huku akiwa amemcharge shs 30,000?
2. Kwanini Dr Longdare wa Mt Meru hospital haku treat issue ya Dorris kama emergency na ampe matibabu pale pale Mt Meru badala ya kupoteza muda na motto kukimbia kwenye idara ya watoto?
3. Kwanini ma nurse wa Levolosi hawakuendelea na jitahada za kuokoa maisha ya Dorris ila walichofanya ni ushahidi tu wakumchoma sindano na kumuwekea oxygen na kisha kwenda kukaa zao ofisi. Nilitegemea mgonjwa mahututi kama huyu angefariki manasi wakiwa wanhangaika huku na kule lakini kwa Dorris ni kinyume kwani kafariki akiwa mikononi mwa mama yake na mimi peke yangu nikiwa pembeni.
4. Baada ya mototo kufariki nikaomba kama naweza pewa mwili ili niupeleke mortuary. Waliniambia kuna gari ya hospitali ndio itakao upeleka mwili wa mototo. Nilisubiri kuanzia saa saba ile mpaka saa 10 za usiku gari haikutokea ndio mwishowe wakaamua kuniruhusu niuchukue mwili wa mjukuu wangu.
5. Tukiwa Levolosi baada ya mototo kufariki mama Dorris alipatwa na uchungu sana na ilimpelekea kuzirai mara tatu. Cha ajabu mama Dorris alipozirai alikuwa anahudumiwa na wagonjwa wenzake na siyo ma Nurse.

SAFARI YA MT MERU HOSPITAL/MORTUARY
1. Tulifika mortuary saa kumi na nusu, tuligonga mpaka saa kumi na moja kasorobo lakini hapakufungukiwa. Wakati huo mkwe wangu mama Dorris yuko kwenye gari amezimia tena.
2. Ilibidi nitoke kuelekea main building ya Mt Meru na nilipofika mapokezi nikamkuta Dr Longdare akiwa amekaa so relaxed pale reception ni kikombe chake cha chai. Nikamwambia nina shida mbili kama ifuatavyo.
Ø Nina motto amefariki hivyo nataka kumpeleka mortuary, hii alinipa maelekezo na nikasaidiwa
Ø Pili mama wa marehemu yuko kwenye amezimia hivyo ninaomba apatiwe matibabu. Dr Longdare huku akiwa pale pale mapokezi na kikombe chake cha chai akasema “aaaaaaaaaaaaaaaa huyu mpeleke tu nyumabi bwana”. Nikamwambia hapana amesha zimia mara tatu akasema “ aaaaaaaaaaaaa kwani kuzimia ni nini bwana? Kweli at that stage I had to lose temper and I asked him what the hell he was doing there. Cha kushangaza aka charge na kuniambia “You must be mother ****er” – imagine loudly. Infact I didn’t know what he meant. Basi baada ya kucharge sana akaniambia mchukue mgonjwa wako mpeleke kule (waliko manesi)
3. Mama Dorris alikuwa amezimia hivyo nilikuwa nahitaji msaada, nilipoenda kwenye chumba cha ma Nurse kuwaomba msaada wakanielekeza sehemu ilipo wheelchair ili nikamlete mgonjwa. Muda wote huo mkwe wangu alikuwa kwenye gari. Nikaendesha wheelchair mwenyewe nikaenda kwenye gari na kuanza kumbeba mama Dorris. Mungu saidia kukatokea watu walioleta wagonjwa wao hivyo walinisaidia kumteremsha mama Dorris na kumpeleka ndani. Note for all that time Dr Longdare was in the same place enjoying his cup of tea.
4. Wakati nampeleka mama Dorris ndani napishana na Nurse mwingine. Nikijua angenisaidia ila aliishia kunikejeli na kusema “Hivi ni nini tena? Nyie hamkwenda Loliondo? Sikumjibu nikaendelea kumsukuma mama Dorris kwenye wheelchair
5. Finally Dr Longdare akaja, akampima mama Dorris na kumuwekea drip mbili mpaka saa moja asubuhi? Je kama hakuwa mgonjwa kwanini alimuwekea drip? Yeye alisema nimpeleke nyumbani?

Bye: Blue Balaa.

Pole sana mkuu, hii habari imenigusa sana, nasikia uchungu maana niliwahi kukutana na same issue.
 
Pole sana ndugu yangu, umenikumbusha nilivoshuhudia bi mkubwa wangu akizidiwa usiku wa manane na hospitali ya AICC Arusha na manesi wakamchoma dawa ya usingizi ili asiwapigie kelele badala ya kutafuta chanzo cha mgonjwa kupiga kelele, kumbe ilikuwa malaria chronic, hakupatiwa vipimo vyovyote hapo AICC, kutokana na dawa ile waliyomchoma, alipoteza fahamu, kukaa kwenye koma wiki mbili na kufariki hospitali ya KCMC. Madaktari KCMC walidai alikuwa na malaria kali sana na shinikizo la damu. Inaniuma hadi leo na nimetokea kuichukia sana ile hospitali. Tuwe makini na hospitali za Arusha.

Yote mwachie Mungu na Time heals the pains, pole pole sana, najua unavyojisikia.

May out little angel Dorice RIP.

Asante sana, AICC ndio hapafai kabisaaaaaaaaaaaaaaa, sijui hata wanafanyaga nini pale. Kifupi ni kwamba Arusha hakuna hospitali
 
Kwanza pole sanaaaa.

Pili, nenda tu kafungue mashitaka rasmi na wakichunguzwa itaonekana uzembe uliofanyika na itakuwa fundisho kwa wote. Juzi Dr amemchoma sindano jamaa yetu akafa hapohapo, sindano wala haina sababu, basi tu. Bahati yao sikuwepo na waliokuwepo waliona - kazi ya Mungu haina makosa (kama wanavyosema wao). Please dont let this pass... Anza na huyo Longdare, hao watu wana miiko yao na taratibu zao, washitaki.
 
Poleni sana mkuu! Mungu awatie nguvu na kuwapa faraja ya pekee kwa familia yote! Hakika inauma sana...poleni sana!
 
Asante sana ndugu, sina details zaidi za Dr Longdare ili that day tarehe 7 past mid night alikuwa ndio Dr wazamu na ma nurse wengine wawili ambao siwajui majina yao. Dr namfahamu kwa sura ni mfupu maji ya kunde. Na kule Levolosi ma nusre siwafahamu kwa majina ili i can identify them. Pia tuli register jina la mtoto kwa kutumia jina lake la utoto GRACE (ambalo ni jina la mke wangu) so the name which was registered is Grace Felix.

Shida ni kwamba Ma Nurse, Madoctor wako SO RELAXED!!!

Wala usijali mkuu hata haya maelezo uliyotoa yanatosha sana hamna noma mkuu...tupo pamoja na hili swala linashughulikiwa wala usijali....zaidi sasa hivi endeleza maombezi kama kawaida....

Again pole sana....
 
Pole sana na familia yote. Thread imenitoa machozi.
May our little angel Dorris rest in peace.
 
Pole sana Blue Balaa na MUNGU muweza yote awape moyo wa uvumilivu.
Tatizo ulilokumbana nalo ni tatizo linalotukumba wengi si Arusha tu bali Tanzania nzima. imefika wakati watoa huduma wanaitoa kwa mazoea badala ya kutumia taaluma zao. hili ni tatizo la system nzima katika serikali na idara zake. lakini inapofikia hata hospitali binafsi nazo zinaingia kwenye mkumbo huo huo basi maisha yetu yapo hatarini sana.
Ndiyo maana mimi sishangai na sintashangaa kuona watu kwa maelfu wakikimbilia Loliondo kwa Babu ili kupata tiba isiyo na masharti na inayotolewa kwa moyo wa huruma na wenye kujenga matumaini mapya kwa wagonjwa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DORRIS MAHALI PEMA PEPONI, AMINA.
 
Pole sana Mkuu. Huu ni uzembe mkubwa ambao umekithiri sehemu zote za huduma za wananchi. Ni wengi sana wamefariki kutokana na uzembe wa madaktari na manesi lakini hatua zozote hazichukuliwi, ndio maana wao wanaona ni kawaida tu na kutukana watu. Tabia hii imeanzia ngazi za juu za serikali hadi kusambaa katika ngazi zote. Hii ni cancer ambayo itaangamiza taifa hatua zisipochukuliwa mapema.
 
Poleni sana, maelfu ya watoto chini ya miaka mitano wanakufa kila siku kwa uzembe wa madaktari na manesi , pneumonia hata ikiwa severe ikapata proper management at a right time watoto wanapona. Hiyo ilikuwa emergency case. Siku hizi hakuna ethics kbsa za kazi. Nimeumia sana, najua machungu yenu hasa mama Dorris. MUNGU wetu aliye hai awatie nguvu na uvumilivu. Kipenzi chetu Dorris apumzike kwa amani.
 
Pole sana Blue Balaa na MUNGU muweza yote awape moyo wa uvumilivu.
Tatizo ulilokumbana nalo ni tatizo linalotukumba wengi si Arusha tu bali Tanzania nzima. imefika wakati watoa huduma wanaitoa kwa mazoea badala ya kutumia taaluma zao. hili ni tatizo la system nzima katika serikali na idara zake. lakini inapofikia hata hospitali binafsi nazo zinaingia kwenye mkumbo huo huo basi maisha yetu yapo hatarini sana.
Ndiyo maana mimi sishangai na sintashangaa kuona watu kwa maelfu wakikimbilia Loliondo kwa Babu ili kupata tiba isiyo na masharti na inayotolewa kwa moyo wa huruma na wenye kujenga matumaini mapya kwa wagonjwa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DORRIS MAHALI PEMA PEPONI, AMINA.

Saharavoice big up, umeongea maneno mazuri sana, Mungu akuzidishie hekima mkuu.
 
Back
Top Bottom