Babra wala si shetani ni MUNGU alitaka kumueleleza huyo bwana anayejifanya muaminifu katika ndoa yake. Unakumbuka mie nilisema juu ya zile sms nilizokuta kwenye simu ya Mr. Mimi pia sikuwa na tabia ya kugusa simu yake hata iite mara mia ila siku hiyo imagine alikuja chicha hajiwezi nikamvua nguo simu nikaziacha kwenye mfuko wa suruali nikapanda kitandani kulala- usingizi hauji, sauti within me inaniambia 'soma messages za Mr. soma , we acha ujinga soma, nakwambia leo hulali soma' dada nilikaa macho one hour najigeuza tu mwenzangu anakoroma- mwisho nikajiuliza kwa nini nikaamka na kuichukua na kuifungua na sms ya kwanza kukutana nayo ni ya huyo hawara yake .... zikafuata na nyingine nyingi.
Na siku zote alikuwa anaimba kuwa akijanikuta au kusikia namegwa na mtu nje ya ndoa ataniua kwa kuwa yeye hamegi. Nikapata pa kuanzia,