-Ni adhabu ipi ambayo itamfaa huyu bazazi zaidi ya Talaka??,what if huyu mama angekufa? maana kumpiga mtu mpaka hatua ya kuzirai ni sawa na kukaribia kumuua,utasema kuna mapenzi hapo home boy,hata kama ni domestic violence hii ni too much bana,ni heri angempiga na baada ya kugundua kuwa kamuumiza angempeleka hospitali kwa matibabu lakini jamaa ndo kwanza kamtelekeza mkewe akiwa katika hali mbaya(mahututi) na mpaka sasa hajulikani alipo,utasema kuna mapenzi hapa??,hapana bana,dawa ni kumuacha tu,huyu jamaa hampendi mkewe ndo maana unaona wakati mkewe akiwa hospitali anasikilizia maumivu ya kipigo na kupoteza ujauzito yeye mume hajulikani alipo(labda anakula raha na nyumba ndogo/kimada wake)
-Kuhusu watoto ndo maana hapo juu niliuliza je wana watoto??,suala la malezi ya watoto isiwe sababu ya kutishia uhai wa wenzi wetu kwa sababu tu twajua hata tukiwapiga na kuwaumiza hawatatuacha kwa sababu ya kuwalea watoto pamoja....Hapana aisee
Babra,rafiki yako anaendeleaje sasa??