Wanabodi, leo kuna msomi mmoja Bw. Kidawi Limbu, amethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, wa Chama cha Wananchi CUF ndie aliyeshinda uchaguzi wa rais wa Zanzibar, amewashangaa wasomi wana kigugumizi gani kuikemea CCM kutaka kulazimisha uchaguzi wa maudio ili waweze kupata ushindi wa bao la mkono!.
Msomi Kidawi Limbu amesema uthibitisho kuwa CUF ndio iliyoshinda, ni matokeo ya uchaguzi uliosimamiwa na NEC kule Zanzibar ambao uchaguzi haukuwa na dosari, katika uchaguzi huo, mgombea wa UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa, alimgaagaza vibaya mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli.
Kwa vile wapiga kura ni wale wale, na chama cha wananchi CUF, kilikuwa ni msharika katika UKAWA, haiwezekani wapiga kura wale wale, wamchague mgombea wa UKAWA kwenye urais wa Muungano na kumpiga chini mgombea wa CCM, halafu wapiga kura hao hao, wakaja kumpigia kura mgombea wa CCM, kwenye uchaguzi wa Zanzibar, hivyo amethibitisha pasi shaka kuwa uchaguzi wa Zanzibar, CUF ilishinda, Maalim Seif Shariff Hamad, ndie rais halali wa Zanzibar ila hajatangazwa!.
Matokeo Rasmi ya uchaguzi ya Urais wa Zanzibar ambayo yanaonyesha wazi kuwa CCM imeshindwa kwa kura nyingi sana kwa kiwango na uzoefu wa Zanzibar, hata kura za Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa upande wa Zanzibar zinaonyesha hivyo hivyo na kwa hiyo kuthibitisha kuwa CCM ilipoteza uchaguzi huo. Kwa muhtasari matokeo ya Urais wa Muungano kwa upande wa Zanzibar ni kama yafuatavyo:
MGOMBEA KURA HALALI ASILIMIA
DR. JOHN POMBE MAGUFULI 194,317 46.5%
EDWARD NGOYAYE LOWASSA 211,033 50.50%
IDADI YA KURA HALALI 417,882
Matokeo ya kura za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani yote yanaonyesha CCM imeshindwa kwa idadi ya kura za walio wengi (popular votes). CCM imeweza kupata viti sawa na CUF katika uwakilishi na ubunge kwa sababu ya mbinu zilizotumika katika ukataji wa majimbo.
Maadam tarehe ya uchaguzi wa marudio imeishatangazwa , na kama ni kweli Seif Shariff Hamad, alishinda, kuna ubaya gani kama CUF watashiriki tena uchaguzi huu wa marudio na kuwa makini sana na bao la mkono, hivyo Maalim Seif Shariff Hamad, si ni atashinda tena?!.
Source: Nimemsikia mwenyewe kwa masikio yangu!.
Pasco