Elections 2015 Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Angalizo walilotoa CCM ni kuwa Nchi haitolewi kwa vikaratasi. Kwa nini wanafuja fedha za umma kwa kufanya maigizo ya uchaguzi?
Hizi fedha zingetumika kujenga vituo vya/nyumba za kulea na kuhifadhi wazee ambao maisha yao yamekuwa Shaghalaghala.
Maalim Seif ameshinda mara zote tangia 1995, ameshashinda mara 5, ashinde tena mara ngapi?

CCM wangeonesha ustaraarabu kwa kukubali(kujifunza) kushindwa.
CCM imekusudia kuleta uvunjifu wa amani.
Nini kilitokea 2001?
 

We kweli hamnazo kama yule mpiga push up wenu.
 
Mkuu,
Huyo bwana Kidawi Limbu ni nani katika medani za kisiasa Zanzibar!?
 
Rafu za kupigana ndondi wajumbe wa tume we kweli POPOMA kuwa ccm inatakiwa ujitoe akili kweli hata reasoning capacity hushuka. KWA TAARIFA YAKO TU NA WANA CCM WENZAKO NI HIVI

KWA ZANZIBAR HATA UCHAGUZI UFANYIKE MARA 100 CCM HAISHINDI
 
Kwa hiyo rafu hizo kwa kuwa walifanya CUF uchaguzi ukafutwa lakini rafu walizofanya CCM huku bara ambazo ziliwekwa wazi na viongozi wa upinzani lakini mbona Lubuva hakufuta uchaguzi?
Vipi kuhusu Bumbuli waliopiga kura kuchagua mbunge walikuwa hawazidi 24,000 lakini waliopiga kura kuchagua Rais wakawa zaidi ya 47,000, je kwa akili yako hicho kilikuwa halali?
 
Mwanakijiji wewe hua nu mdini na hua huipendi CUF machafuko yakitokea urudi ukasuluhishe. Ushauvua utanzania haya ya huku hayakuhusu ongelea ya Donald Trupm ndo saiz yako
 
Yaani toka Mwanakijiji ahamie upande wa "shetani" hata kukemea maovu ya "shetani la rangi ya kijani" hana!! Na hata damu ikimwagika atafurahi tu

Siku hizi tunapata uchambuzi toka kwa akina Pasco. Kudos brother Pasco
 
...naifananisha hali hii ya kutoamini kurudia uchaguzi zenj na wakati wa uchaguzi wa jimbo dogo la arumeru pale nassari alipopambana na nguvu ya ccm na kushinda kwa kishindo...pamoja na kwamba aliwekewa mazingira magumu mno kushinda lakini watu wake walimpa kura....Hivyo napo zenj nashauri kama itabidi uchaguzi urudiwa basi nguvu yote ya ukawa wakiwemo kina lowassa na mbowe wakapige kambi unguja na pemba wahamasishe wapenzi wa cuf kujitokeza kupiga kura bila kuzira.....maana wakizira wakaacha kupiga kura ccm watashinda kwa goli la mkono mapema....maana uchaguzi hauangalii nani alijitokeza kupga kura ama la bali unaangalia matokeo ya mwisho...

...hivyo chinde cuf na ukawa nadhani kwa vile imeshatangazwa siku ya kura basi wahamasishe watu wao watoke kwa wingi kama ilivyokuwa mwanzo na wapige kura kwa umakini na kulinda wizi wa kura usiku na mchana...na ikiwezekana waweke mawakala makini walinde kura....Kwa kifupi cuf watumie mbinu za kina lema, mdee, nassari, mbowe na hata lowassa na wengine walioshiriki chaguzi zenye changamoto ya wizi wa kura ....Ni kwa kufanya hivi tu cuf watashinda....bila hivyo wakifanya kosa la kuzira wataipa ushindi wa chee ccm ambao wanategemea sana kuzira kwa wapiga kura wa upinzani wakati wa marudio ya uchaguzi.....hili limeonekana sana kwenye chaguzi za marudio bara.....cuf wasifanye kosa la kuzira...bali wajipange kupigania kura zao mwanzo mwisho...Mungu atawapa ushindi kwa namna hii....amen....
 
Sasa mkuu swali langu ni kwanini cuf au anyone hawajaenda mahakamani???
 
unambiwa kura pemba zilikua zimezidi idadi walioandikishwa. nini implication yake? ni kwamba wapemba wamepiga kura zaidi ya mara moja au mamluki waliletwa. sasa hii ndio kura za lowassa kuzidi magufuli. sijaona nini unashangilia kama data yako ni kaulu ya huyo limbu.
 
Una ushahidi Wa hilo !!?? Wacha kufanya Wa Tanzania ni wajinga .wewe unatetea ulicho ambiwa .lakini unakataa ushahidi ulioletewa !!!??
 
Limbu anasema kweli hatimae wasio haki watakima tu, ushabiki wa kifedhuri kama wa washabiki wa ccm kuna siku utakoma tu. Waovu huonekana kama hawatakuwa na mwisho wawapo kwenye zama zao, lakini hatimae watakoma tu.
 
CUF wakikubali kurudia CCM watatangaza kabla hata uchaguzi haujaisha subrini wadau mtaona. Kama bado wapo wazanzibari wanachekea na kufurahia kutawaliwa na bara waendelee hakuna haja ya kufanya uchaguzi mwingine atangazwe Shein basi. Mpk wazanzibar wote waamue watabaki kama Haiti iko chini ya Watawala wababe mpk leo. Kuonewa kwa kisingizio cha amani wakikatae wote. WANAFIKI KIBAO
 
We kaka wacha unafik na uongo, pemba ccm hana kiti hata kimoja miaka mingi ccm hawajafanikiwa kupata kiti hata kimoja pemba, na mara hii idadi ya watu walozuwiwa kupiga kura ni kubwa sana, walikuwa na tamaa sana ccm kuwa mara hii watapata kiti japo kimoja pemba kwa sababu kipindi cha uchaguzi walihonga pesa sana lkn matokeo yake watu walikula pesa na kura hawakupewa, bao la mkono kwa chama cha upinzani si rahisi ukizingatia wao ndo wasimamizi wakuu, sababu ya kurejewa uchaguzi ni kuwa ccm wanataka ushindi kama wasemavyo wenyewe ushindi kwao ni lazma, sisi wapemba hatuwezi kuchakachua kwa sababu tunajiamini pemba ccm hana lake, na kama wanasema pemba ndiko kulikotokea matatizo kwa nini wasifanye uo uchaguzi wao uko pemba tu ayo maeneo uloharibiwa? Waongo wezi ccm iko bongo tu lkn kwa znz ktk asilimia 100 basi ccm wakifika ni 35 percentage
 

Kana kwamba haitoshi, walimteka kwa nguvu makamu wake aliekua anaendelea kutangaza matokeo wakati mwenyekiti hajulikani alipokua hadi pale alipokuja kusikika kwenye vyombo vya habari akifuta uchaguzi.

Hata kama uchaguzi wa Pemba ungekua una dosari kila kituo cha kupigia kura, si wangerudia Pemba kisha wakajumuisha na Unguja yaliyoenda sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…