ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Akijiamni kuwa haitatokea siku mambo yakawa hadharani, Mzee ambae mtaani tunamheshimu hali yake ni mbaya sana, presha inamsumbua. Kisa alikuwa na nyumba ndogo binti wa staili ya kuitwa mwanafunzi (sidanganyiki), alimpangia chumba na kuzaa nae kwa siri aliendelea kutoa huduma.
Kumbe wakati wakila raha, wakati fulani binti alichukua namba ya simu ambayo Mzee aliiandika "home" sammbamba na simu ya mzee huyu wa makamo.
Wiki tatu zilizopita, Mzee alikuwa amesafiri kikazi nje ya nchi na hakuweza kumwaga binti (nyumba ndogo kuwa atasafiri). Kutokana na binti kusumbuliwa na matatizo ya kulea mtoto na matumizi na kodi ya nyumba, alipoona anashindwa kumpata mzee, aliamua kupiga namba ambayo aliipata katika simu ya mzee siku za nyuma ile imeandikwa "home". Katika kupiga, mama mwenye nyumba, mke wa ndoa wa mzee anapokea simu na kuuliza wewe nani, binti hakuwa na ajizi akajitambulisha mimi ni mchumba wake mzee fulani, mama akashtuka lakini hakutaka makeke, akamuuliza upo wapi, binti akajibu alipo, mama akasema basi mimi ni dada yake, binti pasipo uelewa akajibu aliwahi kuniambia anaishi na watoto na dada zake tu na mkewe wa ndoa waliachana zamani sana.
Mama akamwambia basi kama unamtafuta, jamaa amesafiri nje ya nchi, ila kama unashida yeyote tunaweza kuoana tu hapana shaka..binti kwa kujua yote sawa, akasema basi ntakutafuta. Kesho yake wakapanga kuonana sehemu, mama akaenda na mdogo wake, kufika wakamkuta binti kawahi, stori, storiiii, binti akaeleza yote kuwa anatembea na mzee muda mrefu, wanamtoto mmoja wa kiume, na mzee alimtenganisha na mpenzi wake ambae walikuwa wote chuoni na waliahidiana kufunga ndoa. Ila mzee walisababisah watengane baada ya siku moja mpenzi wa huyi binti kumfumamina binti na mzee. Binti akaeleza pia kuwa walishawahi kutembelea ameneo wanayoishi mzee na dada zake ila ilikuwa usiku. Mama mwenye ndoa yake akavumilia tu...baada ya maongezi hayo akamtoa binti na vijisenti kidogo vya matumizi na akamwambia akirejea (mzee) atamjulisha.
Siku kama mbili baadae mzee akarejea, mama akasubiri mapka jumapili iliyofuata, mzee yeye ni mtumishi mzuri wa kristo (mzee wa kanisa), siku hiyo ya jumapili walienda kanisani, baada ya kutoka kanisani mama anamwomba Baba Paroko waambatane nae nyumbani, wakati huo mzee alikuwa akihesabu sadaka kanisani...kabla ya hapo mama akampigia simu yule binti, akamwambia mzee kaja njoo, ukifika sehemu fulani panda bodaboda..kisha uliza kwa Mzee fulani watakuelekeza. Binti akasema nakuja fasta kwa kuwa sipo mbali na mitaa hiyo.
Mama na Paroko walipofika nyumbani, muda mchache mzee anaingia akitokea kanisani, akashangaa kidogo kumwona Paroko, lakini hakujali sana kwa kuwa mama nae ni mzee wa kanisa hivyo akidhani ni maswala ya maombezi tu yatafuata na mtumishi huyo wa kiristu.
Wakiwa wanajiandaa kwa chakula, mara mlango ukagonjwa, ghafla binti anaingia kwa mbwembwe asijuie hili wala lile, anashtuka kumwona Paroko na Mzee, anamsalimia mzee kwa tabasamu, mzee nae anashtuka sana ...Mama mwenye nyumba anahamaki, anamwomba binti akae chini, mzee anataka kusimama, mama anamkalisha chini (unakwenda wapi??)..Paroko anashangaa...ghafla mama anamwomba samahani Paroko na kumwambia binti "mimi ndie mke wa ndoa wa huyu Mzee hapa..haya eleza yote uliyonieleza siku ile.." Binti anaogopa sana na kuanza kueleza yote..huku akitoa ,machozi....Baada ya kuhitimisha..Paroko anataka kuingilia kati kuhusu "utaratibu"....mama anamuuliza "haya mzee ipoje..wewe jitu zima na wajukuu unaenda kuzaa na binti mdogo kama huyu??...Mzee anajiumauma ..ghafla anataka kunyanyumka ..anapamua mdomo lakini anashindwa ..anaanguka chini anazimia..(Presha imepanda).
Wiki sasa mzee hali yake ni mbaya, Mama anauguza kwa shingo upande..Hali ya mzee inachangiwa na fedheha iliyoipata mbele ya Paroko na watoto wake. Bado yu hoi kwa Presha...Binti aliruhusiwa kuondoka bila kudhuriwa ..mama alieleza kuwa binti hana kosa lolote na akamuonya asithibutu kuwaamimi wazee wa umri ule kuwa hawana watoto au ndo.