Pamoja na madudu ya wazi na unyanyasaji ambao umekuwa sehemu kubwa ya legacy ya CCM, wamejificha kwenye kichaka cha kuwa chama kilichoikomboa nchi na historia ya Mwalimu Hayati Julius Kambarage Nyerere kunufaisha wachache na kutumia nguvu kutisha wananchi na rushwa kununua wasanii wakubwa ili kuongeza uungwaji mkono. Lakini wakati ni ukuta. Ubabe wao wa kutumia taasisi kurubuni watu haki na kuendeleza mfumo wa unyanyasaji umefika mwisho. Mwaka 2015 Wazanzibari walishuhudia wizi wa kura pale Maalim Seif alipokosa kutangazwa mshinidi licha ya kushinda uchaguzi visiwani Zanzibar.
Mama Samia naye, kwa kuongopea makada wa chama akakubali kuendeleza huu utumbo kwenye uchaguzi wa 2025, yaani CCM haioni haya wala vibaya.
Ikitokea wamepona kutoka na hizi harakati kuna mambo mawili ambayo yanaweza kutokea: Wataminya uhuru wa kujieleza na kuendeleza mfumo wao wa kibabe ukiacha mbali na kutumia dola kunyanyasa upinzani hata zaidi au wataaanza mchakato wa kutafuta katiba mpya ambayo itatanua wigo wa demokrasia na uhuru wa wananchi.
Ikitokea kwamba CCM imetoka madarakani, basi huu ndio utakuwa mwisho wa chama cha CCM na chama kitachukiwa kuliko KANU ya Kenya. Hasa kama upinzani ukichukua madaraka watafanya mageuzi ambayo yataboresha maisha ya wananchi na uhuru wao wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na kulinda rasilimali za nchi.