Imetosha sasa, ni wakati muafaka Rais Ruto kuchukua hatua za makusudi za kimamlaka kuwadhubiti wahalifu nyuma ya Gen z na kurejesha amani

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni dhahiri sasa,

Kumbe nia na dhamira ya vijana wahalifu nyuma ya Gen Z haikuwa kupinga ushuru, kodi, na tozo zilizokuwako kwenye muswada wa sheria ya fedha kwa mwaka 2024/2025 ulioipitishwa na Bunge la Kenya.

Muswada ule umefutwa tayari na Mh. William Samoei Ruto.

Ni nini kingine mnahitaji ambacho hamkukisema awali?

Motisha za kisiasa wanazopewa na viongozi wa kisiasa wenye maoni na mitazamo tofauti na serikali iliyoko madarakani zaidi sana zitawaathiri ninyi wenyewe na maisha yenu ya sasa na wakati ujao. Hilo hamuwezi kulikwepa hata ashushwe malaika kuongoza Kenya, ushuru na kodi lazima mlipe.

Uporaji, ujambazi, wizi wa mali, na uharibifu wa mali na miundombinu vitahitaji nguvu na jitihada zenu za hali na mali kuirejesha katika hali ya kawaida, hilo nalo hamuwezi kulikwepa.

Ni wakati muafaka sasa, Rais Ruto kureact na kukomesha hekaheka hizi za majambazi wanaojificha nyuma ya Gen Z, ambazo sasa hazina kichwa wala miguu.

Wanao watuma wanafahamika. Leo kuna mmoja hata kwenye press conference ya chama chake alitoroka kwa haraka bila kusema neno wakati press ikiendelea.

Wanasiasa walio nyuma yao, na wanaowafadhili na kuwachochea kwa hali na mali, wanajaribu kujificha lakini haiwezekani. Mkono wa sheria ni mrefu, macho ya vyombo vya habari na teknolojia yako wazi, na wengine ni wazoefu wa kuchochea mambo haya ya vurugu na walionusurika mpaka huko ICC.

Itoshe tu kusema, kudeka huku kwa wahalifu nyuma ya Gen Z kumepita kiwango cha uvumilivu na sasa ni wakati muafaka kuchukua hatua kali kuwadhibiti wasiendelee kuharibu nchi.

MUNGU IBARIKI KENYA,

ASANTE PLO LIMUMBA KWA USHAURI MWANANA KWA WAKENYA WOTE.

PIA SOMA
- Gen Z watawanyika katika Makanisa mbalimbali kuzuia Harambee za Wanasiasa kesho, Padre wa Rais Ruto aonywa!
 
Ruto atangaze hali ya hatari haraka iwezekanavyo,mwisho kuonekana nje ni saa kumi na mbili jionii, ukionekana baada ya jionii unaliwa kichwa bila huruma! Maana hao mafala wakianza magonvi yao ya kikabila ,mwisho wa siku yanakimbilia huku Tanzania, alafu kama Raishuweziachaa mali za wananchiwasiokua na hatia kuharibiwa!![emoji1241]!!
 
Huko ndio kukomaa kidemokrasia sasa..
Hapo lazima viongozi watawaheshimu wananchi sana.
 
Huko ndio kukomaa kidemokrasia sasa..
Hapo lazima viongozi watawaheshimu wananchi sana.
kuheshimiana na Lazima,
Lakini pia tabia hii si nzuri kwasababu inaonyesha yeyote yule akitawala Kenya akitoza ushuru na kodi tu wataanza kuandamana kudai atoke madarakani, watauna with nonstop, na haitawasaidia hata kidogo πŸ’
 
Si mda taifa letu litaanza kupokea wakimbizi
sure,
wakifanikiwa kumbandua Ruto madarakani, Lazima sura ya maandamano ibadilike na kua ya kikabila na hapo sasa mauaji na umwagaji damu wa kiholela wa kikabila utaibuka na wenye hofu kuanza kutangatanga na kutafuta penye amani pa kukimbilia ikiwa ni pamoja na Tanzania πŸ’
 
anavyowaacha bila kuchukua hatua kali, wanapata nguvu zaidi na kudeka zaidi. He must act πŸ’
 
Endekeza democary ufe mapema , Ruto angewafinya mapema wahamashaji yasingetokea , hapo jobless na wezi wameupatia ni mwendo wa kuharibu na kufanya uwizi .
 
Napendekeza wauane zaidi Ili akili ziwakae sawa
 
Hayo maduka yanayovunjwa kwa kuvamiwa yanahusika vip !? kama sio ujinga .

Msiombe yakatokea maandamno hapo kariakoo , sinza , kinondoni watu watavunja maduka yenu na kuiba kila kitu . kuna vijana kibao ambao ni jobless watatumia mwanya huo kufanya uhalifu
 
sure,
kukataa musuada wa Sheria ya fedha ilikua geresha tu kumbe walikua na mambo mengine moyoni zaidi ya hilo πŸ’

kwasababu kuvunja, kupora na kuiba maduka na nyumba za wabunge panahusika vipi tena na musuada wa fedha, hali ya kua muswada wenyewe umeshaondolewa bungeni?πŸ’
 
Hao wanatumia mwanya wa maandamano kuvuruga nchi , hii sio sawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…