Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni dhahiri sasa,
Kumbe nia na dhamira ya vijana wahalifu nyuma ya Gen Z haikuwa kupinga ushuru, kodi, na tozo zilizokuwako kwenye muswada wa sheria ya fedha kwa mwaka 2024/2025 ulioipitishwa na Bunge la Kenya.
Muswada ule umefutwa tayari na Mh. William Samoei Ruto.
Ni nini kingine mnahitaji ambacho hamkukisema awali?
Motisha za kisiasa wanazopewa na viongozi wa kisiasa wenye maoni na mitazamo tofauti na serikali iliyoko madarakani zaidi sana zitawaathiri ninyi wenyewe na maisha yenu ya sasa na wakati ujao. Hilo hamuwezi kulikwepa hata ashushwe malaika kuongoza Kenya, ushuru na kodi lazima mlipe.
Uporaji, ujambazi, wizi wa mali, na uharibifu wa mali na miundombinu vitahitaji nguvu na jitihada zenu za hali na mali kuirejesha katika hali ya kawaida, hilo nalo hamuwezi kulikwepa.
Ni wakati muafaka sasa, Rais Ruto kureact na kukomesha hekaheka hizi za majambazi wanaojificha nyuma ya Gen Z, ambazo sasa hazina kichwa wala miguu.
Wanao watuma wanafahamika. Leo kuna mmoja hata kwenye press conference ya chama chake alitoroka kwa haraka bila kusema neno wakati press ikiendelea.
Wanasiasa walio nyuma yao, na wanaowafadhili na kuwachochea kwa hali na mali, wanajaribu kujificha lakini haiwezekani. Mkono wa sheria ni mrefu, macho ya vyombo vya habari na teknolojia yako wazi, na wengine ni wazoefu wa kuchochea mambo haya ya vurugu na walionusurika mpaka huko ICC.
Itoshe tu kusema, kudeka huku kwa wahalifu nyuma ya Gen Z kumepita kiwango cha uvumilivu na sasa ni wakati muafaka kuchukua hatua kali kuwadhibiti wasiendelee kuharibu nchi.
MUNGU IBARIKI KENYA,
ASANTE PLO LIMUMBA KWA USHAURI MWANANA KWA WAKENYA WOTE.
PIA SOMA
- Gen Z watawanyika katika Makanisa mbalimbali kuzuia Harambee za Wanasiasa kesho, Padre wa Rais Ruto aonywa!