ukinuna nuna tu ila mambo ya chumbani usiyanunie, manake yanaweza yakakugharim. Lakini ukweli kwa wwnye ndoa wengi mara chache unaweza ukaamka ukawa hata hutaki kuongea na mwenzio na hii iko kwa wote wawili. yaani ke /me. lakini tujiulize kama mtu umezaliwa na una ndugu zako wa damu, ninyi mlimyonya titi moja, mkala pamoja, mkaoga na hta kulala baba yenu ni mmoja na mama ni mmoja na ipo siku mnanuniana au hata kugombana sembuse huyu mwenzio mliokutana wote mkiwa na meno 32? kila mmoja anatoka kwake? siyo rahisi bwana. angalia hata wanao tu wanaweza wakanuniana au wakagombana sasa je ninyi mliokutana ukubwani si zaidi? haya mambo yapo ila busuara na hekima hasa ya mama ndippo inapotumika zaidi kwani inabidi ajishushe sana ili kurudisha amani hapo ndani kwani always mama ni pambo la nyumba na huwa anapamba nyumba kwa amani, usafi, furaha na lishe bora.