Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
Hivi karibuni tulikutana na Mtaalamu mmoja kutoka Cuba. Alitueleza kwamba huko kwao VVU na Ukimwi siyo tatizo kwa sababu mfumo wao afya unafuatilia kila mtu na kama kuna mgonjwa anashughulikiwa ipasavyo. Atahamishiwa kwenye kituo maalumu na kupewa ushauri nasaha kwa kipindi kirefu hata miezi miwili kabla ya kurudi nyumbani. Pia anafuatiliwa muda wote na madaktari. Hii inasaidia kupunguza maambukizi kwa watu wengine. Lakini kikubwa alisema kuwa wananchi wameelimika na kwamba hakuna ngono bila kondom labda kwa wanandoa tu. Pamoja na ulegevu wa mfumo wa afya hapa kwetu lakini nadhani hilo la pili ndilo lenye mgogoro mkubwa. Wanafunzi wanaacha shule kwa ajili ya mimba, utoaji mimba upo juu na ngono uzembe zinaendelea. Tunaweza kujaribu?