Imewezekana Cuba: Hakuna ngono bila kondom....

Imewezekana Cuba: Hakuna ngono bila kondom....

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Hivi karibuni tulikutana na Mtaalamu mmoja kutoka Cuba. Alitueleza kwamba huko kwao VVU na Ukimwi siyo tatizo kwa sababu mfumo wao afya unafuatilia kila mtu na kama kuna mgonjwa anashughulikiwa ipasavyo. Atahamishiwa kwenye kituo maalumu na kupewa ushauri nasaha kwa kipindi kirefu hata miezi miwili kabla ya kurudi nyumbani. Pia anafuatiliwa muda wote na madaktari. Hii inasaidia kupunguza maambukizi kwa watu wengine. Lakini kikubwa alisema kuwa wananchi wameelimika na kwamba hakuna ngono bila kondom labda kwa wanandoa tu. Pamoja na ulegevu wa mfumo wa afya hapa kwetu lakini nadhani hilo la pili ndilo lenye mgogoro mkubwa. Wanafunzi wanaacha shule kwa ajili ya mimba, utoaji mimba upo juu na ngono uzembe zinaendelea. Tunaweza kujaribu?
 
Hili nalo jambo!!
Si huwa wanasema condomu
zinawawasha!?
 
Hili nalo jambo!!
Si huwa wanasema condomu
zinawawasha!?


Ukizitumia kama dawa hutajali. Ndio maana pamoja na uchungu wote quinine bado inanywewa na kuna watu waliipenda Chloroquine. Nadhani ni suala mindset. Kama akili bado inafikiria upande mwingine hayo unayoyasema na mengine mengi lazima yatazuka tu.
 
Hili nalo jambo!!
Si huwa wanasema condomu
zinawawasha!?
Hii kitu kwakuwa sio natural lazima ina some disadvantages zake. Kikubwa ni kupima consequences za kutumia na kutotumia.
Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia ni mwiko kwake kutumia mpira kwasababu hapati enjoyment nikamshangaa maana nyumba ndogo kila kona.
Ila kali kabisa kuna mama mmoja mtu mzima tu aliwahi kunipa darasa la jinsi ambavyo condom inawasumbua wanawake wengi, I was amazed. From there I sensed perhaps majority dont like the thing.
Pamoja na ugumu wa kukubali waziwazi, idadi kubwa ya watu huwa wanaenda bila mipira na ndio maana mambo yako hivi tunavyoyaona. Inataka kueleweshwa sana tujue athari za uchaguzi zetu.
 
Mpaka hapa tulipo elimu kuhusu namna ya kujikinga na VVU imemfikia kila mtanzania. Lililobaki ni mtu mwenyewe kuamua atumie au asitumie na awe tayari kupokea matokeo ya matendo yake
 
Mpaka hapa tulipo elimu kuhusu namna ya kujikinga na VVU imemfikia kila mtanzania. Lililobaki ni mtu mwenyewe kuamua atumie au asitumie na awe tayari kupokea matokeo ya matendo yake

Mkuu sasa watu hawatumii. Na pia hizo kondom zingesaidia kupunguza mimba zisizotakiwa. Tatizo ni nini? Hapo ndipo tunapohitaji uzoefu wa wadau. Mimi natumia sana kondom kwa ajili ya kupanga uzazi (birth control). Ni zaidi ya miaka 2 sasa na sina tatizo nazo. Ndio maana nashindwa kuelewa kwa nini watu wengine hawatumii? Can anyone educate me pleeeeaase!!!
 
Back
Top Bottom