Alnadaby
JF-Expert Member
- Sep 28, 2006
- 505
- 41
Mizani zetu zinazopima uzito ma magari ni mradi bora zaidi kwa wenye kutamani utajiri wa haraka haraka.Mafisadi vidagaa watarajiwa jiungeni katika wizara husika ili mkusanye hela ya bure.
Jana tanki la mafuta lenye uwezo wa kubeba lita 10,000 lilikuwa likisafirisha mafuta na lilipofika Nyanguge likakuta mzani wa mkeka.Tanki limefanyiwa calibration na watu wa vipimo lina capacity ya 10,000 litres basi hakuna zaidi.
Sasa kasheshe ya Nyanguge hiyo jana ati gari ikwa imezidi uzito.Dereva maskini hana hela.Anajua kuwa watozaji wa mzani wanataka wapewe chakula lakini hana.
Na maskini hakujua taratibu za pale mahali.Kumbe hapo ni sehemu ya biashara na iwe gari imezidi au hakuizidi biashara ni kuwaona wapimaji kwanza.
Poor guy alipoteza muda mwingi akampigia simu tajiri naye akamtosa,na mwisho mwa yote kaambiwa alipe faini shs.800,000/-
Faini hana,mfukoni alipewa allowance shs 20,000 ili aweze kula safarini na kulaza ubavu wake.Anajua kuwa uzito haukuzidi lakini hana jeuri ya kupambana nao na wao ni ma expert wa kucheza na mzani.
Mwisho wa yote sijui alifika au hakufika.Mimi nilijipitia hapo kimya lakini moyoni nikawa najiuliza....hivi haya mamizani yao yakiwa sawa au si sawa nani anajua huko Nyanguge?
Hawa jamaa wa Tanroads nao si ni katika ile familia ya mafisadi?Gari ile ile imepita mizani zote lakini ikifika hapo..inaongezeka uzito..Jamani!!! he..!!
Maisha bora kwa kila fisadi troup...na wasiokuwa wanachama tutaishi vipi?