IMF: Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Uganda Kufikia 11% Kuanzia Mwaka 2025 Baada ya Pesa za Mafuta Kuanza Kumiminika

IMF: Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Uganda Kufikia 11% Kuanzia Mwaka 2025 Baada ya Pesa za Mafuta Kuanza Kumiminika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Shirika la Fedha za Kimataifa IMF imesema Uchumi wa Uganda utaanza kupata Ukuaji mkubwa kuanzia mwaka 2025 ambapo Kasi ya Ukuaji wa Uchumi itaongezeka kutoka asilimia 6.2% mwaka 2024 na kufikia asilimia 10.8% kuanzia mwaka 2025.

Ukuaji huo utachangiwa na kuanza Kumiminika Kwa pesa za mauzo ya Mafuta mwishoni mwa mwaka 2025.

Kasi hii kubwa ya Uchumi wa Uganda itakuza Ukubwa wa Uchumi wa Nchi hiyo kutoka GDP ya $ 49bln (2024) Hadi GDP ya $ 120bln (2035) ambapo Wachambuzi wa Uchumi wanasema Uchumi huo utalingana Kwa Ukubwa na Tanzania.👇👇

View: https://x.com/Reuters/status/1834128627794931796?t=rBXwRZpnNB7hhcOWwp-hJQ&s=19

My Take
Kuna haja ya Tanzania kwenda kujifunza Kwa Ethiopia iliwezaje kukuza Uchumi wake Kwa double digit Kwa miaka 10 na kuzipita Kenya,Angola na Sudani kuwa Baba wa Uchumi Afrika Mashariki huku hawana Mafuta Wala gesi.
Screenshot_20240916-182313_1.jpg

Vinginevyo Tanzania tutapitwa na Uganda Kwa Ukubwa wa Uchumi (GDP size) baada ya mwaka 2035.

Nchi zote ambazo zilipata maendeleo makubwa ni zile ambazo Uchumi wake uliwahi kujua Kwa double digit yaani kuanzia 10% Kwa miaka 10 mfululizo Duniani kote ndipo zilipunguza umaskini Kwa nusu vinginevyo Hali itazidi kuwa tete.

Hii growth rates ya 4-7% ambayo tumekuwa nayo Kwa miaka zaidi ya 15 haijawahi na Wala haitakuja saidia kuondoa umaskini 👇👇

View: https://x.com/TanzaniaInvest/status/1833424456926044371?t=OuBdrDykvfYDPafDjZrbMg&s=19

Pia soma World Bank: Rwanda, Uganda na DRC zitaongoza kwa Kasi ya Ukuaji wa Uchumi Afrika Mashariki. Tanzania kushika nafasi ya 3.

Pia soma zaidi hapa WB: Uchumi wa Tanzania (GDP) Umeongezeka na kufikia $ 80 Bilioni mwaka 2023.
 
Ubaya li chama lako la kijani ndilo liko madarakani miaka na miaka ila suala dogo tu hilo la kukuza uchumi kwa double dijit wameshindwa. Lakini kila kukicha machawa mnalisifia, acheni unafiki li chama lenu hilo haliwezi kutufikisha popote pamoja na kuwa na rasilimali na fukwe kubwa karibia nchi nzima.
 
Swala la Chama Cha CCM kuwepo Madaraka sio ishu hata kama ingekuwa Chadema,Cha muhimu ni watu waje na mapendekezo ya muhimu ambayo Serikali iyape kipaombele.

Sio kama Ile ya dira ya Taifa ya Kuoa sijui ujinga gani mlikuwa mnatoa maoni.
 
Ni lini dira ya taifa ilifanya kazi Tanzania?
Kina chotumika kuongoza taifa la Tanzania ni ilani ya chama cha Mapinduzi ambapo pamoja na kuitunga ninyi wenyewe ila hamjawahi kufikia target hata ya 60% ya mambo mlioahidi kukamilisha kwenye ilani yenu. Hii ni aibu kubwa
 
Hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania ambayo ina gas nyingi lakini kutokana na CCM kukosa maono, hakuna lolote la maana. Msumbiji ni miongoni mwa nchi 10 za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa haraka.

Kwa huo ukuaji wa 11% wa Uganda, ni karibia mara 4 ya ule wa Tanzania. Tanzania itabakia kuwa mtazamaji.
 
Pole ,kwani Kwa Sasa hakuna mchakato wa kukusanya maoni ya dira ya Taifa ya 2050 unaendelea?
 
Hii ni habari mbaya sana kwa Tanzania ambayo ina gas nyingi lakini kutokana na CCM kukosa maono, hakuna lolote la maana. Msumbiji ni miongoni mwa nchi 10 za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa haraka.

Kwa huo ukuaji wa 11% wa Uganda, ni karibia mara 4 ya ule wa Tanzania. Tanzania itabakia kuwa mtazamaji.
Sio mara 4 Bali ni mara 2 ya Ukuaji wa Tanzania kama takwimu zinavyoonesha hapo Juu.
 
Bro unakuwa kama hauishi Tanzania!
Kubali kwamba mdololo wa uchumi Tanzania ni kutokana na chama tawala!
Ingekuwa chama gani ndio Uchami ungekuwa vizuri? Ni kweli vipaombele vya Tanzania chini ya CCM vina ukakasi sana ila walau Kwa Sasa naona Mwanga awamu hii ya 6 Kuna utofauti kwenye sera kiasi Fulani.
 
2025, kataa ccm , okoa rasilimali za Taifa na uhai wa nchi yetu

Tumeliwa vya kutosha

CCM ndio ya kulaumiwa kwa matokeo yote, umasikini na ujinga uliokithiri, chanzo ni CCM, ilaaniwe na kila mtu mwenye akili timamu
 
Back
Top Bottom