IMF: Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Uganda Kufikia 11% Kuanzia Mwaka 2025 Baada ya Pesa za Mafuta Kuanza Kumiminika

IMF: Kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Uganda Kufikia 11% Kuanzia Mwaka 2025 Baada ya Pesa za Mafuta Kuanza Kumiminika

Sasa utaongeza GDP per Capita bila kuongeza GDP size?

Mapesa ambayo Uganda itavuna kwenye Mafuta yanaenda kuwekeza kwenye Huduma za jamii na Uchumi hivyo kuwarahisishia Waganda kuongeza vipato Vyao.
Mkuu hayo mapato ya mafuta Tanzania nayo ina share yake tena kubwa sana kwa kupitisha bomba la mafuta kwenye ardhi yake mbona hamyasemi?
Hii nchi ya Wagalatia nani aliwapa roho mbaya hadi mnachukia mkono wako wa kushoto japo ni kiungo chako cha mwili wako?
Kama hamuipendi nchi yako hamia Syria.
 
Shirika la Fedha za Kimataifa IMF imesema Uchumi wa Uganda utaanza kupata Ukuaji mkubwa kuanzia mwaka 2025 ambapo Kasi ya Ukuaji wa Uchumi itaongezeka kutoka asilimia 6.2% mwaka 2024 na kufikia asilimia 10.8% kuanzia mwaka 2025.

Ukuaji huo utachangiwa na kuanza Kumiminika Kwa pesa za mauzo ya Mafuta mwishoni mwa mwaka 2025.

Kasi hii kubwa ya Uchumi wa Uganda itakuza Ukubwa wa Uchumi wa Nchi hiyo kutoka GDP ya $ 49bln (2024) Hadi GDP ya $ 120bln (2035) ambapo Wachambuzi wa Uchumi wanasema Uchumi huo utalingana Kwa Ukubwa na Tanzania.👇👇

View: https://x.com/Reuters/status/1834128627794931796?t=rBXwRZpnNB7hhcOWwp-hJQ&s=19


My Take
Kuna haja ya Tanzania kwenda kujifunza Kwa Ethiopia iliwezaje kukuza Uchumi wake Kwa double digit Kwa miaka 10 na kuzipita Kenya,Angola na Sudani kuwa Baba wa Uchumi Afrika Mashariki huku hawana Mafuta Wala gesi.
View attachment 3097657

Vinginevyo Tanzania tutapitwa na Uganda Kwa Ukubwa wa Uchumi (GDP size) baada ya mwaka 2035.

Nchi zote ambazo zilipata maendeleo makubwa ni zile ambazo Uchumi wake uliwahi kujua Kwa double digit yaani kuanzia 10% Kwa miaka 10 mfululizo Duniani kote ndipo zilipunguza umaskini Kwa nusu vinginevyo Hali itazidi kuwa tete.

Hii growth rates ya 4-7% ambayo tumekuwa nayo Kwa miaka zaidi ya 15 haijawahi na Wala haitakuja saidia kuondoa umaskini 👇👇

View: https://x.com/TanzaniaInvest/status/1833424456926044371?t=OuBdrDykvfYDPafDjZrbMg&s=19

Pia soma World Bank: Rwanda, Uganda na DRC zitaongoza kwa Kasi ya Ukuaji wa Uchumi Afrika Mashariki. Tanzania kushika nafasi ya 3.

Pia soma zaidi hapa WB: Uchumi wa Tanzania (GDP) Umeongezeka na kufikia $ 80 Bilioni mwaka 2023.

Hatimaye hela za Mafuta zimeanza kuleta matokeo kama tulivyosema Pato la taifa la Uganda (GDP) yaizidi ya Tanzania kwa mwaka 2025 kwa mujibu wa shirika la fedha duniani -IMF
 
Back
Top Bottom