#COVID19 IMF yaidhinisha mkopo wa Tsh Trilioni 1.2 kwa ajili ya Corona Tanzania

Ushamaliza maendeleo? Kwa akili zako finyu unaona ni ndio pesa hiyo ya kumaliza matatizo ya Tzn?

Huna akili hiyo pesa hata km 1000 za lami haitoshi ila kwa umbumbumbu wako unaona ni pesa nyingi sana
We mataga embu tulia acha jazba,wapi nimesema hiyo pesa inaweza maliza matatizo yote Tz!? Au umekurupuka na hangover!?
 
Ebu sema kwanza mama kaikuta hazina na kiasi gani ndiyo ushutumu hiyo mikopo.
 
Ebu sema kwanza mama kaikuta hazina na kiasi gani ndiyo ushutumu hiyo mikopo.
Mbona alishasema? Au wenzetu huwa hamfatilii wala kusikiliza?
Alisema Kuna dollar 3.5bil, na akasema nchi inauwezo wa kujiendesha miezi 6
 
Zinakopwa, wajanja wanazipiga, sisi ma boli zozo,, tutakamuliiwa zilipwe
 
Deni la Taifa itakuwa linakaribia trillion 75 sasa. Nilifikiri tozo zingetufanya tuache kukopa?!
 
Mbona zote Dar tu ? Kwingine si .....Tanzania ? Vipi Kigoma....kwa VP
 
Sasa itakuwa na Lissu alikuwa anazunguka kwa wazungu akiwaambia wasiwape msaada Tanzania.
 
Mbona zote Dar tu ? Kwingine si .....Tanzania ? Vipi Kigoma....kwa VP
Kule wanajengewa project kubwa ya kupeleka umeme wa gridi. Project nyingi ndogo ndogo tunazimudu kwa pesa za ndani. Ila hizi project kubwa ndo inabidi kupata nguvu ya wahisani.
 
Siyo ku double ni kuweka rehani resource zetu. Ogopa.
 
Sidhani kama hata wanaamini kama kuna sekta zilizokwama kwa ajili ya corona....ingekuwa hivyo si wangeachana na tozo ili iwe ndio nafuu ya Wananchi kwa mdororo wa kiuchumi?.
Huo ndio ukweli...Corona wanaiimba tu wakitaka mikopo, lakini wala hawaamini kama ipo... mama mwenyewe juzi umemsikia anauliza kama watu wachanje wasichanje? Wakati alituaminisha kuwa tumuunge mkono tuchanje.
 
Katiba mpya si dawa! Katiba za nchi zinasimamishwaga. Lazima tutafute kiini cha matatizo, mimi nafikiri tatizo kubwa ni umaskini. Rais atakayefanikiwa kuondoa umaskini au kuwapa wananchi unafuu wa maisha- afya bora, maji yanapatikana , watoto wanaenda shule, vijana wanashughuli za kuwaingizia kipato, vijana wanaenda sekondari na vyuo vikuu, wazee wanapata matibabu ya bure, wafanyibiashara wanafanyabiashara bila kubugudhiwa, wawekezaji wanakuja kuwekeza, fedha inazunguka mikononi mwa wazawa- ndio muhimu zaidi. Nchi yetu ijikite kuondoa umaskini . Katiba mpya ni muhimu katika kupunguza madaraka ya Rais- na kuunda tume huru ya uchaguzi. Sidhani kama mtu wa hali ya chini hicho ndio kipaumbele chake cha kila siku.
 
Point ila sasa huo umaskini tutauondoaje ingali serikali iliyotuongoza miaka 60 imeshindwa kutuondolea umaskini na bado wanang'ang'ania madaraka!!!?bila Katiba mpya itakayo tupatia tume huru ya uchaguzi nadhani umaskini utatutafuna mpaka kiama.
 
Kukopa muhimu ila mkopo huu karibu Tilioni 1 plus ni WA masharti nafuu na unalenga kukuza uchumi.

Pili utaleta nafuu unadhani kukibana mkanda ni mchezo mkuu.Binafsi nimefurahia Cha msingi tuu tuuelekeze kwenye sekta zalishi
Mjinga tu ndo anaweza kufurahi, CCM na maendeleo wapi na wapi?
Zaidi kila leo ni tozo tozo.
 
Hii mikopo huko tuendako kutaanzishwa tozo yakupumua ili tulipe madeni,sio kwa ukopaji huu ths z too much!
Deni la taifa kwa Sasa n zaidi ya 70trln na bado tunaendelea kukopa huku tunaongeza tozo zakizalendo!
 
Hizo Tozo za madilu zinaenda wapi??
Kama kila mwizi msaada na mikopo.
Hunaweza kuta hata mishahara ya wafanya kazi tunakopa.
Hii ni Anguko kubwa kwa taifa.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Sasa kama tozo kwa mwezi haifiki billion arobaini kwa mwezi, ikimaanisha kwa mwaka ni wastani wa bilioni miatano. Sasa bilioni miatano kwa mipango ya nchi nayo ni pesa ya kupigia kelele namna hyo
 
Ni za bure ama kuna kuzirudisha?
 
Tatizo tunaotaka kuwakabidhi nchi wamekimbilia kwa hao wanaotupa hii mikopo.. Kiufupi sioni ukombozi wowote kutoka upinzani.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…