REDEEMER.
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 8,925
- 14,890
Shirika la fedha duniani (IMF) limetoa wito kwa serikali ya Kenya kuchukua hatua za dharura kudhibiti ongezeko la deni la kitaifa ambalo sasa linakadiriwa kukaribia asilimia 60 ya pato la taifa.
Mwakilishi wa IMF nchini Kenya, Jan Mikkelsen ameonya kuwa kuongezeka kwa mkopo wa taifa kutaathiri vibaya bajeti ya taifa, shughuli za benki nchini na hatimaye kusababisha wakopeshaji kusita kutoa mikopo zaidi. “Tunatoa wito kwa serikali ya Kenya kuanza mikakati ya kudhibiti ongezeko mkopo wa taifa,” Mikkelsen alisema jijini Nairobi. Alieleza wasiwasi kuwa uchumi wa Kenya haukui kwa kasi ya kuweza kuzalisha fedha za kutosha kulipa deni ambalo sasa ni asilimia 57 ya pato la taifa.